Watu 552 waliokuwa wameambukizwa Corona nchini Iran wapona
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i59560-watu_552_waliokuwa_wameambukizwa_corona_nchini_iran_wapona
Iran imetangaza kuwa hadi sasa watu 552 waliombukizwa ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama Corona wamepona na wamepewa ruhusa ya kurudi nyumbani kutoka hospitali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 05, 2020 06:10 UTC
  • Watu 552 waliokuwa wameambukizwa Corona nchini Iran wapona

Iran imetangaza kuwa hadi sasa watu 552 waliombukizwa ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama Corona wamepona na wamepewa ruhusa ya kurudi nyumbani kutoka hospitali.

Akizungumza na waandishi habari Jumatano hii mjini Tehran, Kianoush Jahanpour mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Umma katika Wizara ya Afya ya Iran amesema watu hao wote waliopona wako katika hali nzuri hivi sasa.

Ameongeza kuwa, hadi kufikia leo Jumatano adhuhuri kulikuwa na kesi mpya 586 za waliombukizwa kirusi cha Corona kote Iran na hivyo kwa ujumla walioambukizwa ni 2,922. Amesema  hadi kufikia Jumatano watu 92 wamepoteza maisha nchini kutokana na kirusi cha Corona. Halikadhalika ametoa wito kwa wananchi wa Iran wasistishe safari zisizo na dharura baina ya miji na pia wajiepusha ni mijumuiko ili kuepusha kuenea ugonjwa huo.

Image Caption

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, hadi sasa zaidi ya watu elfu 95 wameathirika na kirusi cha Corona kote duniani ambapo kati yao watu elfu 45 wamepona huku wengine zaidi ya 3,286  wakifariki dunia. Korea Kusini na Italia ni kati ya nchi zilizoathriwa zaidi na kirusi cha Corona baada ya China ambapo hadi sasa watu 107 wamepoteza maisha Italia kutokana na ugonjwa huo huku walioambukizwa Korea Kusini wakifika 5,766.

Marekani pia inaonekana kuathiriwa vibaya baada ya jimbo la California kutangaza hali ya hatari huku hadi sasa watu 11 wakiripotiwa kufariki dunia nchini humo kutokana na kirusi cha Corona.  

Iran iko mstari wa mbele kwa kufanya kazi usiku na mchana katika kupambana na kirusi hicho kinachoenea kwa kasi. Wataalamu nchini Iran wako mbioni kuunda chanjo ya kirusi cha Corona aina ya COVID-19 na inatarajiwa kuwa katika siku zijazo watatangaza mafanikio katika uga huo.