Iran, nchi yenye uwezo mkubwa katika masuala ya afya
Shirika la Afya Duniani (WHO) linaitambua Iran kama nchi yenye uwezo mkubwa katika masuala ya afya na ina mawasiliano na ushirikiano mazuri sana, mkubwa na dhati na shirika hilo kuhusu ugonjwa wa Covid-19.
Waziri wa Afya na Tiba wa Iran, Saeed Namaki ameeleza kuwa mfumo wa huduma za afya na matibabu wa Iran katika eneo la magharibi mwa Asia ni wa aina yake na kuongeza kuwa: Iran ina uzoefu mzuri kama vile katika kutokomeza ugonjwa wa kupoooza viungo (polio), surua, kudhibiti malaria, tetenasi na magonjwa mengine mengi ya kuambukiza.
Wizara ya Afya ya Iran imekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya virusi vya corona kwa juhudi zisizoweza kusahaulika ambazo ni ishara ya uwezo wa mfumo wa afya na matibabu wa Iran kwa ajili ya kutokomeza virusi hivyo hatari. Shirika la Afya Duniani pia limeiarifisha sekta ya matibabu na afya ya Iran kuwa moja ya mifumo yenye nguvu kubwa ya kiafya katika eneo la mashariki mwa Mediterania. Taasisi za masuala ya sayansi na teknolojia nchini Irani, sambamba na wafanyikazi wa sekta ya afya na tiba hapa nchini, zimekuwa ikifanya juhudi kubwa na zenye taathira tangu siku za kwanza za kukabiliana na Corona. Matunda muhimu yaliloshuhudiwa katika mchakato huo kupitia taasisi hizo ni kutengeneza kifaa ambacho teknolojia ya uzalishaji wake ulikuwa ukimilikiwa na nchi chache zilizoendelea.
Sorena Sattari, Makamu wa Rais wa Iran anayeshughulikia masuala ya sayansi na teknolojia ameeleza kuwa mashirika ya utafiti wa sayansi yanafanya utafiti wa kutengeneza dawa za kutibu corona. Ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kwamba: Kazi inafanywa sasa kuanzia utengenezaji wa mitambo ya kutengeneza barakoa, dawa za kuua vijidudu maradhi hadi vifaa vya kisasa kabisa vya tiba kama mashine za kusaidia kupumua (ventilators), vifaa vya vyumba vya ICU, mashine za CT scan, uzalishaji wa vifaa vya kupima virusi vya corona na vilvie zinafanyikaa jitihada za kupata chanjo na dawa ya virusi hivyo kupitia makundi matatu ya kujitegemea.
Hii leo, utambuzi na upimaji wa virusi vya corona unafanywa kwa kutumia vifaa vilivyotengenezwa Irani, na haya ni matokeo ya kazi nzuri ya mashirika ya utafiti katika sekta ya akili bandia (Artificial intelligence (AI))na stawi wa uwezo wa vituo vya utafiti wa kielimu ya kisayansi hapa nchini.
Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona duniani hadi sasa imepindukia milioni mbili na laki saba na watu karibu laki mbili miongoni mwao wameaga dunia. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, maambukizi ya ugionjwa wa Covid-19 ni janga la dunia nzima na kwamba kukabiliana na virusi vya corona ni mtihani mkubwa kwa nchi zote duniani. Sekta za afya na matibabu katika aghalabu ya nchi duniani na hata huko Marekani na barani Ulaya zimeathiriwa na matatizo makubwa katika miezi kadhaa iliyopita hasa baada ya kuanza mlipuko wa maambukizi ya corona duniani. Utengenezaji wa barakoa au maski, glovu, vifaa vya afya na dawa za kujikinga na maambukizi ni miongoni mwa changamoto hizo kubwa. Kwa upande mwingine ni kuwa, hakuna wataki maalumu wa kuondokana na hatari ya maambukizi ya Covid-19. Kwa msingi huo, kazi muhimu zaidi katika kipindi cha sasa ni kuharakisha utambuzi wa waathirika wa corona, kuwaweka karantini na hatimaye kukata mnyororo wa maambukizi ya virusi hivyo.
Maambukizi ya virusi hivi vya corona wamewahamasisha wasomi na watafiti katika nchi mbalimbali kufanya juhudi kubwa za utafiti. Miongoni mwa kazi zilizofanywa na watafiti wa Kiirani katika uwanja huo ni pamoja na kuanzisha utengenezaji wa barakoa za nano hadi utafiti wa ya kutengeneza chanjo ya virusi hivyo.
Masoud Suleimani msomi na mwanasayansi wa Kiirani amezungumzia chunguzi unaofanyika hapa nchini kwa kutumia seli shina za wagonjwa waliopatwa na corona na kueleza kuwa: Utafiti huo unafanyika katika hospitali mbili za Shariati na Masih Daneshvari chini ya usimamizi wa Naibu Waziri anayehusika na utafiti katika Wizara ya Afya; matokeo ya awamu ya kwanza ya majaribio yatatangazwa karibuni na Wizara ya Afya.
Katika mazingira haya, kubadilishana taarifa za kitiba kuna umuhimu mkubwa kwa ulimwengu, na Iran iko tayari kuzipatia nchi nyingine mafaniko, tajiriba na uzoefu wake katika kukabiliana na corona. Nchi nyingi zinashirikiana na kusaidiana katika uwanja huu isipokuwa Marekani ambayo kwa vikwazo vyake dhidi ya Iran na hata kulikea vikwazo Shirika la Afya Duniani, imeudhihirishia ulimwengu jinsi inavyoendelea kujitenga na kuwa mbali zaidi na thamani na sifa za kibinadamu.