Zarif: Marekani ni nchi ya kwanza duniani inayoziadhibu nchi zinazotii sheria
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa siasa za mabavu za Marekani ambayo yenyewe imekiuka mapatano ya nyuklia ya JCPOA na wakati huo huo inatumia mabavu kuzilazimisha nchi nyingine zikiuke sheria na kufuata nyayo zake.
Muhammad Javad Zarif ameashiria lsera za vitisho za Marekani katika kadhia ya makubaliano yya nyuklia yya JCPOA na kueleza kuwa: Washington si tu imekiuka mapatano hayo bali inazilazimisha nchi nyingine zifanye hivyo. Zarif ameongeza kuwa Marekani imekuwa nchi ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa kubeba fedheha ya kuziwekea vikwazo nchi zinazotekeleza sheria hususan azimio nambari 2231 la Uumoja wa Mataifa.
Rais Donald Trump wa Marekani Jumanne Mei 8 mwaka juzi alichukua msimamo wa upande mmoja na kukiuka majukumu ya Washington kwa mujibu wa mapatano ya JCPOA na kutangaza kuiondoa nchi hiyo katika mapatano hayo ya kimataifa. baada ya hatuua hiyp Trump alianza kutekeleza vikwazo vya nyuklia dhidi ya Iran.
Srikali ya Trump imekuwa ikitoa vitisho kwa jamii ya kimataifa kutokana na jitihada zake za kuyalinda mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kuheshimu azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hatua hiyo ya Trump imelaaniwa na kukosolewa pakubwa na jamii ya kimataifa.
Maria Zakharova Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia hivi karibuni ameeleza namna Moscow ilivyotilia mkazo udharura wa kuyalinda mapatano ya nyuklia ya JCPOA mkabala na mashambulizi makali ya Marekani na kusisitiza kuwa: kulindwa mapatano ya JCPOA na kudhamini utekelezaji kamili wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kunawezekana kwa juhudi za pamoja za nchi zote.