Zaidi ya wagonjwa 259,000 wa Covid-19 nchini Iran wamepata afueni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i62492-zaidi_ya_wagonjwa_259_000_wa_covid_19_nchini_iran_wamepata_afueni
Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema, wagonjwa wengine wapya wapatao elfu mbili wa maradhi ya Covid-19 wamegunduliwa nchini, huku idadi ya waliopata afueni ya ugonjwa huo ikipindukia 259,000.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 29, 2020 10:31 UTC
  • Zaidi ya wagonjwa 259,000 wa Covid-19 nchini Iran wamepata afueni

Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema, wagonjwa wengine wapya wapatao elfu mbili wa maradhi ya Covid-19 wamegunduliwa nchini, huku idadi ya waliopata afueni ya ugonjwa huo ikipindukia 259,000.

Sima Sadat Lari, Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran ameyaeleza hayo leo wakati akitoa takwimu mpya za watu waliokumbwa na virusi vya corona hapa nchini Iran na akabainisha kuwa: Kwa mujibu wa matokeo ya vipimo rasmi, katika muda wa saa 24 zilizopita wagonjwa wapya 2,636 waliokumbwa na ugonjwa wa Covid-19 wamegunduliwa hapa nchini, ambapo 1,604 miongoni mwao wamelazwa hospitali na waliosalia wamepatiwa huduma za tiba na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Bi Lari amefafanua kuwa, idadi ya watu waliougua ugonjwa wa Covid-19 nchini Iran imefikia 298,909 na kutokana na wagonjwa 196 kuaga dunia katika kipindi cha saa 24 zilizopita, jumla ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo hadi sasa imefikia 16,343.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran hadi kufikia leo mchana, wagonjwa 259,116 wamepata afueni na kuruhusiwa kutoka hospitalini na kurejea majumbani.

Hayo yameripotiwa huku idadi ya watu waliokumbwa na virusi vya corona duniani kote ikifikia 16,920,000. Miongoni mwa hao, watu wasiopungua 664,000 wameshaaga dunia na wengine zaidi ya 10,485,000 wamepata nafuu na kuruhusiwa kutoka hospitali.../