Zarif: Silaha za Atomiki za Marekani na Israel ni tishio kwa eneo
-
Mohammad Javad Zarif
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa kauli kwa mnasaba wa siku ambayo Marekani ilidondosha mabomu ya atomiki huko Hiroshima Japan wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na kusema jinamizi la silaha za atomiki linapaswa kufika ukingoni.
Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran siku ya Alhamisi aliandika ujumbe kwa mnasaba wa mwaka wa 75 wa shambulizi la atomiki la Marekani dhidi ya mji wa Hiroshima nchini Japan katika siku za mwisho za Vita vya Pili vya Dunia na kusema: Miaka 75 iliyopita katika siku kama hii, Marekani ilipata sifa mbaya ya kuwa nchi ya kwanza na ya pekee ambayo imewahi kutumia silaha za atomiki ambazo ziliwalenga watu wasio na hatia."
Zarif amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ni kati ya wamiliki wakubwa zaidi wa silaha za atomiki katika eneo la Asia Magharibi na kuongeza kuwa: "Leo silaha za atomiki za Marekani na Israel ni tishio kwa eneo."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa wito wa kuhitimishwa utengenezaji na urundikaji wa silaha za atomiki duniani. Aidha ametoa wito wa kihitimishwa jinamizi la silaha za atomiki na itikadi ya kuangamizana kwa silaha za atomiki.