Mousavi: kubadilishwa "Brian Hook" hakutaleta mabadiliko katika siasa za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i62679-mousavi_kubadilishwa_brian_hook_hakutaleta_mabadiliko_katika_siasa_za_marekani
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa kubadilishwa Briah Hook aliyekuwa mjumbe maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran hakutabadilisha chochote siasa za nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 07, 2020 23:54 UTC
  • Mousavi: kubadilishwa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa kubadilishwa Briah Hook aliyekuwa mjumbe maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran hakutabadilisha chochote siasa za nchi hiyo.

Sayyid Abbas Mousavi aliyasema hayo jana baada ya kubadilishwa kwa aliyekuwa mjumbe maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran.  Mousavi ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: Hakuna tofauti kati ya Brian Hook mjumbe maalumu wa Rais wa Marekani katika masuala ya Iran, John Bolton mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa serikali ya Washington na shakhsia wengine wenye misimamo mikali wa chama cha Republican kuhusiana na siasa za Marekani kwa ajili ya kukabiliana na Iran. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa: Hali ni hiyo hiyo kwa Mike Pompeo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Rais wa nchi hiyo Donadld Trump na viongozi wengine wajao baadaye. wa Marekani. 

Brian Hook juzi usiku alitangaza kujiuzulu wadhifa wa mjumbe maalumu wa Rais wa Marekani katika masuala ya Iran. Hook ni mmoja kati ya wanasiasa mashuhuri wa Marekani waliopinga mapatano ya nyuklia ya Iran (JCPOA) na kufanikisha utekelezaji wa siasa za mashinikizo ya kiwango cha juu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Hata ivyo siasa hizo zimefeli katika malengo yake ya kuiburuta Iran kwenye meza ya mazungumzo na kufikia mapatano mengine kwa maslahi ya watawala wa sasa wa White House. 

Brian Hook, Mjumbe Maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran aliyejiuzulu siku ya Alhamisi