Araqchi: Ni muda wa pande nyingine husika ndani ya JCPOA kuchukua maamuzi
(last modified Mon, 28 Jun 2021 02:31:47 GMT )
Jun 28, 2021 02:31 UTC
  • Sayyid Abbas Araqchi
    Sayyid Abbas Araqchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, sasa ni wakati wa pande nyingine husika ndani ya mapatano ya JCPOA kuchukua maamuzi, na kwamba nchi hizo zinapasa kuchukua maamuzi magumu.

Sayyid Abbas Araqchi ameashiria kikao chake cha jana Jumapili na wanachama wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ndani ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na kueleza kuwa: Amefanya mashauriano na wawakilishi wa kamisheni hiyo kuhusu mazungumzo ya Vienna yanavyoendelea. 

Kuhusu matokeo ya mazungumzo hayo, Araqchi amesema, hadi kufikia sasa zimeshafanyika duru sita za mazungumzo na kundi la 4+1 na kwamba mazungumzo hayo takriban yanakaribia marhala ya mwisho. Amesema, sasa umewadia wakati kwa nchi husika ndani ya mapatano ya JCPOA kuchukua maamuzi. 

Mazungumzo ya JCPOA mjini Vienna Austria 

Mazungumzo kuhusu mapatano ya JCPOA yamekaribia katika awamu yake ya mwisho baada ya kufanyika duru sita za mazungumzo ya kina na endelevu huko Vienna, mji mkuu wa Austria. 

Lengo kuu la mazungumzo hayo ni kuhuisha mapatano ya nyuklia yaliyodorora baada ya Marekani kujiondoa kinyume cha sheria katika makubaliano hayo na kukiuka sheria za kimataifa.

Tags