Uwezo wa Jeshi la Iran ni sababu ya maadu kutoihujumu nchi hii
Brigedia Jenerali Ahmad Reza Pourdastan, Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwepo tayari kivita jeshi la nchi hii ni sababu kuu inayowazuia maadui kuitishia Iran.
Kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Pourdastan, jeshi la nchi kavu la Iran liko tayari kikamilifu kulinda mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu.
Aidha amebainisha kuwa jeshi la Iran linafuatilia kwa karibu vitisho nje ya mipaka ya Iran na hivyo haliwezi kukabiliwa na vitisho vya kushtukiza.
Brigedia Jenerali Pourdastan amesema jeshi la Iran linaimarisha mafundisho ya nadharia za kijeshi, silaha mpya na misingi ya kiimani ili kuongeza uwezo wake wa kivita.
Amesema adui hawezi kutekeleza vitisho vyake dhidi ya Iran kutokana na uwezo mkubwa wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu.