Marekani: Tuna wasiwasi kuhusu mafanikio ya roketi ya kubeba satalaiti la Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i78650-marekani_tuna_wasiwasi_kuhusu_mafanikio_ya_roketi_ya_kubeba_satalaiti_la_iran
Marekani imetangaza kuwa ina wasiwasi kuhusu mafanikio ya roketi ya kubeba satalaiti katika anga za mbali ya Simorgh nchini Iran.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Dec 31, 2021 01:22 UTC
  • Marekani: Tuna wasiwasi kuhusu mafanikio ya roketi ya kubeba satalaiti la Iran

Marekani imetangaza kuwa ina wasiwasi kuhusu mafanikio ya roketi ya kubeba satalaiti katika anga za mbali ya Simorgh nchini Iran.

Ikulu ya Rais wa Marekani, White House, jioni ya Alkhamisi ya jana ilitangaza wasiwasi wake juu ya kurushwa kwa roketi ya kubeba satalaiti ya Simorgh nchini Iran, na kudai kuwa itaendelea kufungamana na mazungumzo ya Vienna.

Itakumbukwa kuwa, Wizara ya Ulinzi ya Iran ilitangaza jana Alkhamisi kuwa imerusha kwa mafanikio roketi ya Simorgh inayotumiwa kupeleka satalaiti katika anga za mbali.

Akitangaza habari hiyo,  msemaji wa Timu ya Anga za Mbali ya Wizara ya Ulinzi ya Iran Sayyid Ahmad Hosseini amesema kuwa, suala la kutengeneza maroketi yenye nguvu za kubeba satalaiti kubwa zaidi katika masafa ya mbali zaidi lilipata nguvu na kuwa moja ya ajenda kuu za wizara hiyo baada ya Iran kupata mafanikio katika kurusha angani satalaiti ndogo kwa kutumia maroketi ya Safir na Ghasedak.

Sayyid Hosseini amesema, sehemu zote zilizohusika na urushaji wa roketi hiyo ya majaribio zimefanya kazi zake vizuri na kufanikiwa kufikia lengo lililokusudiwa.

Roketi la kubeba satalaiti katika anga za mbali la Simorgh 

Amesema, katika operesheni ya utafiti ya satalaiti iliyotumwa angani kwa kutumia roketi ya Simorgh, ni mara ya kwamba kurushwa vifurushi vitatu vya utafiti kwa wakati mmoja katika umbali wa kilomita 470 kwenda angani na kwa kasi ya mita 7350 kwa kila sekunde.

Roketi ya kubeba satalaiti la Simorgh la Iran lina uwezo wa kurusha satalaiti zenye uzito wa kilo 250 katika mzunguko wa kilomita 500 wa ardhi.