Jan 01, 2022 03:33 UTC
  • Kuondoka Marekani katika eneo, sehemu ndogo ya matokeo ya kuuawa shahidi Soleimani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema kufungasha virago na kuondoka vikosi vya jeshi la Marekani katika eneo la Asia Magharibi ni sehemu ndogo ya matokeo ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika taarifa jana Ijumaa, wizara hiyo imesema kwa mnasaba wa kukaribia mwaka wa pili tangu alipouawa shahidi Soleimani kwamba, serikali ya Marekani inabeba dhima ya kimataifa ya kuuawa kidhulma shujaa huyo wa kupambana na ugaidi.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imebainisha kuwa, hatua ya maafisa wa Marekani kujitokeza hadharani na kukiri wazi kuwa Washington ndiyo iliyotekeleza mauaji hayo, ilidhihirisha wazi kuwa watawala wa Marekani wanaunga mkono magenge ya kigaidi.

Imesema ukatili huo kwa mara nyingine tena ulianika peupe jinai za Marekani, ambayo daima imekuwa ikiihadaa jamii ya kimataifa kuwa ipo mstari wa mbele kupambana na magenge ya kigaidi duniani.

Hajj Soleimani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran iimesisitiza kuwa, watawala wa Marekani waliokuwa uongozini kipindi hicho cha kuuawa kigaidi shahidi Qassem Soleimani, wanapaswa kuwajibishwa kwa jinai hiyo ya kutisha, ambayo ni mfano wa wazi wa ugaidi wa kiserikali.

Shahidi Soleimani ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kikatili la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. 

Tags