Iran yalaani kimya cha jamii ya kimataifa kuhusu mauaji ya polisi Wairani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i78732-iran_yalaani_kimya_cha_jamii_ya_kimataifa_kuhusu_mauaji_ya_polisi_wairani
Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu Iran amekosoa kimya na kutochukua hatua taasisi za kimataifa kuhusu mauaji ya maafisa wa polisi wa nchi hii wanaopoteza maisha katika mapambano dhidi ya magaidi, wafanya magendo wenye silaha na magenge.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 02, 2022 04:36 UTC
  • Iran yalaani kimya cha jamii ya kimataifa kuhusu mauaji ya polisi Wairani

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu Iran amekosoa kimya na kutochukua hatua taasisi za kimataifa kuhusu mauaji ya maafisa wa polisi wa nchi hii wanaopoteza maisha katika mapambano dhidi ya magaidi, wafanya magendo wenye silaha na magenge.

Katika barua kwa Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Kazem Gharibabadi Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu Iran amesema baadhi ya nchi zinafuatilia sera za undumakuwili na kisiasa katika kukabiliana na makundi ya kigaidi na wafanya magendo ya kimataifa.

Gharibabadi amesema tokea Machi 21 hadi Disemba 3 mwaka 2021, maafisa 40 wa polisi wa Iran wameuawa wakati wakipambana na wahalifu na wafanya magendo ambao huwa wamejizatiti kwa kila aina ya silaha.

Aidha ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina azma imara katika mapambano dhidi ya wafanya magendo ya dawa za kulevya, wanadamu na bidhaa na imekuwa moja ya nchi zilizofanikiwa zaidi duniani katika mapambano hayo. Gharibabadi amesema azma ya Iran ya kukabiliana na uhalifu huo imepelekea nchi hii kupata hasara kubwa ikiwa ni pamoja na kuuawa shahidi maafisa 3,800 wa usalama na kujeruhiwa wengine 12,000 katika vita dhidi ya wafanya biashara haramu ya dawa za kulevya.

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Haki za Binadamu Iran amesema anataraji Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa atalaani vikwazo haramu na  vya upande mmoja  dhidi ya watu wa Iran hasa katika kuwapa polisi wa Iran zana za kukabiliana na magaidi na wafanya magendo wa kimataifa.