Ripota Maalumu wa UN: Kuna udharura wa kukomesha vikwazo dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i88082-ripota_maalumu_wa_un_kuna_udharura_wa_kukomesha_vikwazo_dhidi_ya_iran
Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa amechapisha ripoti yake rasmi kuhusu ulazima wa kukomesha vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 12, 2022 10:43 UTC
  • Ripota Maalumu wa UN: Kuna udharura wa kukomesha vikwazo dhidi ya Iran

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa amechapisha ripoti yake rasmi kuhusu ulazima wa kukomesha vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Iran.

Katika ripoti yake, Alena Douhan, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa, amegusia uchunguzi wa athari mbaya za vikwazo nchini Iran.

Alena Douhan alikuwa katika safari ya siku 11 hapa nchini Iran iliyokuwa na lengo la kuchunguza athari mbaya za vikwazo vya upande mmoja vya Marekaqni kwa wananchi wa Iran. 

Kwa mujibu wa ripoti rasmi ya Douhan, vikwazo hivyo vilipanuka na kuingia katika sekta ya nishati na sekta nyingine muhimu za kiuchumi.

Ripoti hiyo imesema, vikwazo dhidi ya sekta ya fedha ya Iran vimeathiri shughuli za Benki Kuu na benki za kibiashara.

Vilevile imeashiria ushirikiano wa nchi za Ulaya na Canada na Marekani katika kuiwekea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Katika safari yake nchini Iran pia Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa alitembelea kituo maalumu cha kutibu watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kipepeo (Lupus). Ugonjwa huo ni ulemavu wa ngozi usio wa kawaida na matatizo mengine ya kiafya yanayoambatana na mateso makali na yasiyotibika na yumkini ukasababisha kifo kwa waathirika.

Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vimekwamisha uagizaji wa dawa za kufubaza ugonjwa huo kutoka nchini Sweden.