Biashara kati ya Iran na Afrika Mashariki imeongezeka kwa 100%
(last modified Tue, 04 Oct 2022 08:01:15 GMT )
Oct 04, 2022 08:01 UTC
  • Biashara kati ya Iran na Afrika Mashariki imeongezeka kwa 100%

Naibu Mkuu wa Shirika la Kustawisha Biashara la Iran amesema miamala ya kibiashara kati ya Jamhuri ya Kiislamu na nchi za Afrika Mashariki imeongezeka kwa asilimia 100 katika kipindi cha miezi mitano iliyopita.

Ahmad-Reza Alaie Tabatabaie amesema hayo na kuongeza kuwa, hatua kadhaa zimechukuliwa kwa ajili kutatua matatizo ya miundomsingi, kama vile kuunda mawasiliano ya kilojistiki baina ya Iran na Oman.

Afisa huyo anayeshughulikia maendeleo ya masoko ya nje amesema shirika lake linatafuta njia za kutekeleza mifumo ya biashara ya kubadilishana bidhaa na washirika wa kibiashara wa bara la Afrika.

Hapo awali alibainisha kuwa shirika hilo limetayarisha orodha ya bidhaa 1,100 ambazo zinaweza kujumuishwa katika biashara ya kubadilishana bidhaa na nchi za Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alipoitembelea Tanzania hivi karibuni

Aidha aliashiria ongezeko la asilimia 45 la mauzo ya bidhaa za Iran barani Afrika, akisema: "Kwa sasa, Ghana ni kituo cha kwanza cha mauzo ya Iran barani Afrika, ikifuatiwa na Afrika Kusini na Nigeria katika nafasi za pili na tatu."

Tabatabaie ameashiria pia biashara kati ya Iran na Pakistan na kubainisha kuwa, ana matarajio kwamba katika miezi michache ijayo, ustawi chanya baina ya mataifa haya mawili ya Kiislamu katika uga biashara utashuhudiwa.

 

Tags