Nov 04, 2022 06:45 UTC
  • Imam wa msikiti auawa katika shambulio la kigaidi mkoani Sistan na Baluchistan kusini mwa Iran

Mkuu wa Polisi wa Sistan na Baluchistan ya Iran amesema: Kabla ya Sala ya Magharibi hapo jana Imamu wa msikiti wa Moulay-e-Mottaqian katika mji wa Zahedan, kusini mashariki mwa Iran, aliuawa shahidi kwa kupigwa risasi na magaidi.

Katika mahojiano na ripota wa shirika la habari la Fars hapo jana, Kamanda Ahmad Taheri alisema: Leo kabla ya sala ya Magharibi na Isha, Hujjat-ul-Islam Sajjad Shahraki, Imamu wa Msikiti wa Moulay-e-Mottaqian mjini Zahedan, alipigwa risasi na magaidi na kuuawa shahidi.
Kamanda wa polisi wa Sistan na Baluchistan ameongeza kuwa: katika uchunguzi wa awali wa polisi imebainika kwamba watu wenye silaha waliokuwa wamepanda magari mawili huku wamefunika nyuso zao na wakiwa wamebeba bastola, walimfyatulia risasi Hujjatul Islam Sajjad Shahraki, Imamu wa msikiti wa Moulay-e-Mottaqian, zilizompata kichwani na kifuani.
Kamanda Ahmad Taheri

Kamanda Taheri amebainisha kuwa: watu hao wenye silaha walikimbia mara tu baada ya shambulio hilo la ufyatuaji risasi; na Hujjatul Islam Shahraki akakimbizwa haraka hospitalini na wafanyakazi wa kituo cha dharura cha huduma za matibabu lakini akafa shahhidi kutokana na majeraha makubwa aliyopata.../

 

Tags