Kiongozi Muadhamu atembelea maonesho ya uwezo wa uzalishaji nchini Iran
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo ametembelea maonyesho ya uwezo wa ndani ya Iran katika nyuga tofauti, ambapo ametumia masaa matatu katika maonyesho hayo.
Kwa mujibu tovuti ya habari wa Ofisi ya Kiongozi Muadhamu, maonyesho haya yanafanyika kwa mnasaba wa kauli mbiu ya mwaka huu wa 1401 Hijria Shamsia ambayo ni "Mwaka wa Uzalishaji Unaotegemea Elimu na Kutengeneza Ajira 1401."
Katika maonyesho haya, uwezo wa ndani katika nyanja za madini na utafutaji, umeme na mawasiliano ya simu, anga na satelaiti, magari, kilimo na chakula, reli, barabara, usafiri wa baharini na anga, sekta ya makazi, mafuta ya petroli na petrokemikali, vyombo vya nyumbani, nguo, viwanda, ufugaji wa samaki, usimamizi wa vyanzo vya maji, viwanda vya kuzalisha nishati na mitambo ya kuzalisha umeme na miradi ya ujenzi wa mabwawa na usimamizi wa maji, teknolojia ya habari na mawasiliano, ulionyeshwa.
Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja mwaka wa 1401 Hijria Shamsia kuwa ni "Mwaka wa Uzalishaji Unaotegemea Elimu na Kutengeneza Ajira" ambapo amesisitiza kuwa kuzingatia maendeleo ya makampuni yanayotegemea maarifa ndiyo njia bora zaidi ya kuunda nafasi mpya za kazi.