Gharibabadi: Kusamehewa watuhimiwa Iran ni ubunifu usio na kifani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i93728-gharibabadi_kusamehewa_watuhimiwa_iran_ni_ubunifu_usio_na_kifani
Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Kibinadamu la Iran amesema kusamehewa watuhumiwa nchini ni ubunifu usio na kifani na kuongeza kuwa: "Hatua hii ya kibinadamu na Kiislamu ni kubwa katika uga wa haki za binadamu na inaonyesha kuwa mfumo wa Kiislamu wa Iran ni wa wananchi na wenye huruma."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 06, 2023 04:33 UTC
  • Gharibabadi: Kusamehewa watuhimiwa Iran ni ubunifu usio na kifani

Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Kibinadamu la Iran amesema kusamehewa watuhumiwa nchini ni ubunifu usio na kifani na kuongeza kuwa: "Hatua hii ya kibinadamu na Kiislamu ni kubwa katika uga wa haki za binadamu na inaonyesha kuwa mfumo wa Kiislamu wa Iran ni wa wananchi na wenye huruma."

Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Kibinadamu la Iran Kazem Gharibabadi ambaye pia ni mkuu wa masuala ya kimataifa katika Idara ya Mahakama ya Iran ametuma ujumbe wa Twitter na kuashiria hatua ya  Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya kuiidhinisha pendekezo la Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran,  la kupunguziwa vifungo au kuachiwa huru makumi ya maelfu ya wafungwa wakiwemo watuhumiwa wa gashia za hivi karibuni nchini zilizoungwa mkono na madola ya kigeni. Katika ujumbe wake wa Twitter Gharibabadi ameandika: "Huu ni ubunifu usio na kifani na ni hatua kubwa katika uga wa haki za binaadamu na inaonyesha kuwa mfumo wa Kiislamu wa Iran ni wa wananchi na wenye huruma."

Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Kibinadamu la Iran ameongeza kuwa: "Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameafiki pendekezo la Mkuu wa Idara ya Mahakama kuhusu kusamehewa makumi ya maelefu ya wafungwa hasa watuhumiwa na waliohukumiwa kufuatia ghasia za hivi karibuni nchini Iran na hivyo mafaili yao ya mahakamani sasa yatafungwa."

Jana Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, alitoa msamaha na punguzo la vifungo kwa makumi ya maelfu ya watuhumiwa na wafungwa waliohusika na ghasia za hivi karibuni. Msamaha huo umetolewa kwa mnasaba wa kuwadia maadhimisho ya miaka 44 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na sikukuu za mwezi wa Rajab.

Hatua ya Kiongozi Muadhamu kuafiki kuafikia pendekezo la kutoa msamaha na punguzo la vifungo kwa watuhumiwa na waliohukumiwa kuhusika na ghasia za hivi karibuni nchini Iran ni nukta muhimu ambayo inaonyesha busara na muono wa mbali wa Kiongozi Muadhamu kwa ajili ya uthabiti wa Mapinduzi na Iran ya Kiislamu.

Katika ghasia za hivi karibuni, maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran walitumia uwezo wao wote kutoa pigo kwa mfumo wa Kiislamu na wananchi, lakini kama ilivyokuwa katika miaka iliyopita, njama hii imesambaratishwa na kwa mara nyingine umoja wa wananchi na nguvu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni nukta mbili ambazo zimepelekea njama hizo kugonga mwamba.