Iran na Uzbekistan zatiliana saini hati kadhaa za ushirikiano
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i98938-iran_na_uzbekistan_zatiliana_saini_hati_kadhaa_za_ushirikiano
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uzbekistan zimetiliana saini hati kadhaa za ushirikiano katika nyanja mbalimbali ambazo zinalenga kukuza zaidi mashirikiano baina ya mataifa haya mawili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 18, 2023 09:51 UTC
  • Iran na Uzbekistan zatiliana saini hati kadhaa za ushirikiano

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uzbekistan zimetiliana saini hati kadhaa za ushirikiano katika nyanja mbalimbali ambazo zinalenga kukuza zaidi mashirikiano baina ya mataifa haya mawili.

Utilianaji saini huo umefanyika leo hapa mjini Tehran baina ya Marais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Shavkat Mirziyoyev wa Uzbekistan aliyeko hapa nchini kwa ziara rasmi.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uzbekistan zimetiliana saini taarifa ya pamoja na hati 10 za ushirikiano katika nyuga mbalimbali.

Hati ya ushirikiano wa kibiashara, usafiri na uchukuzi, kilimo, ushirikiano wa dawa, bima na teknolojia ni miongoni mwa mambo yaliyotiwa saini na pande mbili kwa minajili ya kushirikiana katika nyanja hizo.

Mazungumzo ya ya Marais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Shavkat Mirziyoyev wa Uzbekistan

 

Mbali na utiaji saini huo, Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uzbekistan wamesisitiza ama na irada ya nchi zao ya kuimarisha na kukuza zaidi ushirikiano katika masuala mbalimbali.

Rais Shavkat Mirziyoyev wa Uzbekistan leo aliwasili hapa nchini akiitikia mwaliko wa mwenyeji wake Rais Ibeahim Rais.

Inafaa kuashiria hapa kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliutambua rasmi uhuru wa Uzbekistan tarehe 25 Desemba 1991 na mwezi Mei mwaka 1992 kukaanzishwa uhusiano wa kisiasa baina ya mataifa haya mawili.