Amir- Abdollahian akaribisha kustawisha uhusiano kati ya Iran na nchi za Kiafrika
Hossein Amir- Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran jana alikutana na kuzungumza na Issa Boro Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Burkina Faso na kukaribisha kustawisha uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi za Kiafrika.
Katika mazungumzo hayom, Hossein Amir-Abdollahian ameashiria harakati za hivi karibuni katika uhusiano kati ya Iran na Burkina Faso na kubadilisha jumbe nchi mbili na kueleza kuwa:Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeliweka katika ajenda yake ya kazi suala la kustawisha uhusiano na nchi za Kiafrika.
Amir Abdollahian aidha amesema kuwa kufanyika mkutano wa kamisheni ya pamoja katika siku zijazo huko Burkina Faso ni fursa nzuri kwa ajili ya kuweka saba uhusiano katika nyanja zote za kiuchumi, kibiashara, kisayansi na kielimu.
Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Burkina Faso pia amesema amefurahishwa na safari yake hapa Tehran na akasema madhumuni ya safari yake hii ni kuchunguza nyanja zenye maslahi kwa nchi mbili khususani mahusiano ya kiuchumi.
Issa Boro aidha amesisitiza kuhusu uamuzi wa serikali ya Burkina Faso wa kufungua tena ubalozi na kutuma balozi mjini Tehran na kuongeza kuwa:mazingira yanayohitajika tayari yameandaliwa ili kuimarisha uhusiano katika nyanja zote kwa kuzingatia azma ya pande mbili ya kustawisha uhusiano kati yazo.