Ayatullah Khamenei: Mapinduzi ya Kiislamu, yameikoa Iran na kuporomoka
Ayatullah Khamenei amesema mbele ya hadhara ya mamia ya akinababa, mama na wake wa mashahidi kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu yameinusuru Iran katika bonde la mporomoko wa maadili, kidini na kisiasa.
Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema leo katika mazungumzo hayo kuwa: Vijana wa Iran wamepigana katika matukio yote baada ya ushindi wa Mapinduzi; na wameipa heshima na fahari Iran kwa kutoa pigo kwa adui katika njama mbalimbali na kwa kubadili vitisho kuwa fursa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amewataja mashahidi kuwa ni mashujaa wakubwa wa historia ya Iran na kubainisha nafasi ya juu ya familia za mashahidi katika pande mbalimbali za Qur'ani, jihadi, ubinadamu na kijamii, na kuwatolea wito wasanii na vyombo vya habari kufanya juhudi zaidi katika kubakisha hai kisanaa kumbukumbu ya mashahidi ili kuwa kigezo kwa ajili ya kizazi cha vijana.
Ayatullah Khamenei aidha amewataja akina baba, mama na wake wa mashahidi kuwa hazina ya kipekee ya kumbukumbu ya mashahidi mashujaa wa kujihami kutakatifu, usalama, kulinda haram na matukufu na kukabiliana na matukio kama yale ya mwaka uliopita na kuongeza kuwa: Nyenendo za mashujaa hao, akhlaqi nzuri, mtindo na matukio ya maisha yao ni kigezo kwa jamii khususan vijana na mabarobaro; ambapo kuenezwa kumbukumbu ya familia za mashahidi kupitia kigezo hiki kuna nafasi muhimu.