-
IRGC: Tutatoa jibu zito kufuatia mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran
Jun 13, 2025 05:21Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, IRGC, limelaani vikali shambulizi la kijeshi lililofanywa na Israel dhidi ya ardhi ya Iran, ambalo limepelekea kuuawa kwa Kamanda Mkuu wake, Meja Jenerali Hossein Salami.
-
Hujuma ya kikatili ya Israel dhidi ya Iran yalaaniwa vikali Kimataifa
Jun 13, 2025 05:15Jumuiya ya kimataifa imejitokeza kwa sauti moja kulaani vikali mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ikitaja kitendo hicho kuwa ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na tisho kubwa kwa amani ya Mashariki ya Kati.
-
Serikali ya Iran yaapa kulipiza kisasi baada ya hujuma ya mashambulizi ya Israel
Jun 13, 2025 05:07Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa tamko kali la kulaani mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel alfajiri ya leo Ijumaa, ambayo kwa mujibu wa ripoti za awali, yamepelekea kuuawa shahidi maafisa waandamizi wa kijeshi pamoja na wanasayansi mashuhuri wa nyuklia wa Iran. Tehran imetaja mashambulizi hayo kama “kitendo cha kigaidi kinachoakisi uoga.”
-
Jenerali Ali Fadavi: Iran itaifanya Israel kujutia mashambulizi yake
Jun 13, 2025 05:03Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Ali Fadavi, amesema kuwa Iran iko tayari kulipiza kisasi kikubwa dhidi ya Israel kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya ardhi ya Iran, akisisitiza kuwa hatua hiyo itaiumiza na kuiaibisha Israel na washirika wake.
-
Iran yaitisha kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia mashambulizi ya Israel
Jun 13, 2025 04:40Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewasilisha ombi rasmi kwa Umoja wa Mataifa ikiitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama, kufuatia kile ilichokiita “kitendo cha wazi cha uchokozi” kilichotekelezwa na Israel dhidi ya ardhi ya Iran.
-
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Kufuatia Mashambulizi ya Leo ya Utawala wa Kizayuni
Jun 13, 2025 01:04Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa rasmi kulaani vikali uvamizi wa kijeshi uliofanywa na utawala dhalimu wa Kizayuni dhidi ya ardhi ya Iran.
-
Taarifa Namba 1 kutoka Makao Makuu ya Majeshi ya Iran
Jun 13, 2025 00:45Kitengo cha Mawasiliano cha Makao Makuu ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimetoa taarifa rasmi kikilaani vikali uvamizi wa wazi uliofanywa na adui muovu wa Kizayuni.
-
Kiongozi Muadhamu: Utawala wa Kizayuni umejiandalia hatima chungu na yenye maumivu
Jun 13, 2025 00:11Katika taarifa ya kulaani shambulio lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ardhi tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mapema leo alfajiri, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ametoa ujumbe mzito kwa taifa la Iran, akisisitiza kuwa adhabu kali inamsubiri mhalifu huyo wa kimataifa.
-
Makamanda wa ngazi za juu wa Iran wauawa shahidi katika hujuma ya Israel
Jun 12, 2025 23:37Meja Jenerali Hossein Salami, kamanda mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), pamoja na Meja Jenerali Mohammad Bagheri, Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Iran wameuawa shahidi katika hujuma ya anga lililotekelezwa na utawala katili wa Israel mapema Ijumaa alfajiri mjini Tehran.
-
Milipuko mikubwa yasikika Tehran na maeneo mengine ya Iran
Jun 12, 2025 23:01Milipuko mikubwa ilisikika mapema asubuhi ya Ijumaa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Iran, Tehran, na pia katika mikoa mingine nchini.