-
Kiongozi Muadhamu: Iran inakataa kabisa sisitizo la kufanya mazungumzo na madola ya kibabe
Mar 09, 2025 01:44Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyid Ali Khamenei, amesema kuwa sisitizo la baadhi ya madola ya kibabe juu ya kufanyika mazungumzo na Iran halilengi kutatua matatizo.
-
Iran: Hakuna mazungumzo na Marekani wakati kuna vitisho na vikwazo
Mar 08, 2025 07:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema Tehran haitashiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja kuhusu nyuklia na Marekani maadamu Washington inaendelea na vikwazo vya upande mmoja na vitisho.
-
Shutuma na bwabwaja za uwongo za Wamagharibi dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran
Mar 08, 2025 07:17Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: Miradi ya nyuklia ya Iran inayofanyika kwa malengo ya amani haiwezi kuangamizwa kwa shambulio la kijeshi. Araqchi ameeleza haya akijibu uropokaji na uwongo wa Wamagharibi dhidi ya miradi ya nyuklia ya nchi hii.
-
Araghchi: Kuundwa nchi moja ya kidemokrasia ndiyo suluhu ya kadhia ya Palestina
Mar 08, 2025 03:32Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesisitiza tena msimamo wa Tehran wa kupinga eti 'suluhisho la mataifa mawili' kuwa njia ya kupata haki za Wapalestina na kusisitiza kwamba, uungaji mkono usioyumba wa Iran kwa kadhia ya Palestina bado upo thabiti.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Mazungumzo na Marekani ni kujidhalilisha
Mar 07, 2025 07:43Imam wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa, kufanya mazungumzo na Marekani ni kujidhalilisha. Amesisitiza kuwa, taifa la Iran ni la hamasa ya Karbala na 'Ashura na kamwe halikubali kudhalilishwa.
-
Iran yateuliwa Makamu wa Rais wa OPCW licha ya upinzani wa Marekani
Mar 07, 2025 07:16Iran imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Utendaji la Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali (OPCW) licha ya Marekani kufanya juu chini kuzuia Jamhuri ya Kiislamu kuteuliwa kwenye nafasi hiyo.
-
Iran: Baraza la Qur'ani la Ulimwengu wa Kiislamu litasahilisha uhusiano na ushirikiano baina ya Waislamu
Mar 07, 2025 04:24Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu la Iran amesema: "kuundwa Baraza la Qur'ani la Ulimwengu wa Kiislamu kunaweza kusahilisha ujengaji wa uhusiano na kubadilishana tajiriba kwa ajili ya ushirikiano kati ya Waislamu."
-
Iran: Kufurushwa Wapalestina Gaza ni muendelezo wa mauaji ya kimbari
Mar 06, 2025 23:03Iran imesema kuwa, mpango wa kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina wa Gaza na kuwapeleka katika nchi jirani ni kuendeleza mauaji ya kimbari kwa kutumia zana za kisiasa.
-
Onyo la Iran kwa Troika ya Ulaya kwa kukiuka Azimio la Umoja wa Mataifa na JCPOA
Mar 06, 2025 23:01Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa yaliyoko mjini Vienna, ametoa indhari kwa Troika ya Ulaya kuhusiana na ukiukaji wake wa Azimio la Umoja wa Mataifa na la Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA.
-
Mjumbe wa Iran IAEA: Kampeni ya mashinikizo ya Magharibi dhidi ya Iran haina tija
Mar 06, 2025 02:17Balozi na Mwakilishi wa Iran katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ameonya kuwa, mkakati wa Magharibi wa kutoa mashinikizo kwa Tehran na kuilazimisha kutekeleza kwa upande mmoja majukumu ya kinyuklia "sio tu kwamba haufanyi kazi bali pia hauna tija" .