-
Jeshi la Iran: Udhibiti wa kimkakati wa Lango-Bahari la Hormuz sasa ni matakwa ya kitaifa
Jul 17, 2026 02:59Msemaji wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa suala la udhibiti wa kimkakati wa Mlango-Bahari wa Hormuz sasa limegeuka kuwa matakwa ya kitaifa, akisisitiza kuwa wananchi wa Iran wanaunga mkono hatua zinazolenga kulinda maslahi na usalama wa taifa katika njia hiyo muhimu ya kimataifa ya usafirishaji wa mafuta.
-
Ebola yazidi kuwa tishio katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Jul 17, 2026 02:57Mlipuko wa maradhi ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unasambaa zaidi ya juhudi zinazochukuliwa za kuudhibiti huku zaidi ya watu 2,000 wakiambukizwa na zaidi ya 750 wakiwa wameaga dunia.
-
Wagonjwa wa saratani Gaza wakabiliwa na uhaba mkubwa wa dawa na vifaa tiba
Jul 17, 2026 02:53Wagonjwa wa saratani katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na hali ngumu kutokana na uhaba mkubwa wa dawa na vifaa vya matibabu, hali inayozidi kuhatarisha maisha yao huku mfumo wa afya ukiendelea kulemewa na athari za mzingiro na vita.
-
Eritrea yajizatiti kukabiliana na tamaa ya Ethiopia; wasiwasi waongezeka kuhusu kurejea mvutano Pembe ya Afrika
Jul 17, 2026 02:48Dalili za kuongezeka kwa mvutano kati ya Eritrea na Ethiopia zimeibua wasiwasi wa uwezekano wa kurejea mgogoro kati ya mataifa hayo mawili ya Pembe ya Afrika.
-
Iran yaonya italenga miundombinu yote ya eneo iwapo miundombinu yake itashambuliwa
Jul 16, 2026 10:51Iran imeonya kwamba italenga kila miundombinu iliyosalia katika eneo hili iwapo miundombinu yake itashambuliwa.
-
Qalibaf: Hakuna sababu ya kuendelea kuzingatia makubaliano na Marekani iwapo Iran hainufaiki
Jul 16, 2026 10:47Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ameonya kwamba ikiwa Jamhuri ya Kiislamu haitanufaika na Mkataba wa Maelewano (MoU) wa Islamabad uliotiwa saini baina yake na na Marekani, basi hakuna sababu yoyote ya kuendelea kuufuata.
-
Wafanyakazi wa kukabiliana na Ebola waandamana DRC wakidai mishahara yao
Jul 16, 2026 10:45Wafanyakazi wa afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameanzisha mgomo kushinikiza kulipwa mishahara na marupurupu yao ambayo hawajapokea, hatua iliyosababisha kusimama kwa shughuli za kukabiliana na virusi vya Ebola vinavyoenea kwa kasi.
-
Iran yakemea shambulio la Marekani karibu na hospitali ya watoto huko Ahvaz
Jul 16, 2026 10:42Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekemea shambulio la Marekani karibu na hospitali ya watoto wanaougua saratani katika mji wa Ahvaz, kusini-magharibi mwa nchi, na kulitaja kuwa ni “uhalifu wa kivita wa kijinga na wa woga.” Taarifa zinasema shambulio hilo lililazimisha uokoaji wa dharura wa mamia ya wagonjwa walio katika hali hatarishi na pia limewatia hofu watoto wanaopatiwa matibabu ya saratani.
-
UN: Zaidi ya watu milioni 48 Afrika Mashariki wako katika hatari ya njaa ya kutisha mwaka 2026
Jul 16, 2026 10:36Shirika la Misaada la Umoja wa Mataifa (UN) limeonya kuwa Afrika Mashariki inaendelea kuwa kitovu cha janga kubwa la kibinadamu, huku watu wapatao milioni 48.5 wakihitaji misaada ya dharura mwaka huu.
-
Mzunguko hatari wa vitisho vya Trump dhidi ya Iran
Jul 16, 2026 09:45Baada ya kushindwa kikamilifu mbinu zake zote za vikwazo, vitisho vya kijeshi na mashinikizo ya kisiasa, vitisho vipya vya Trump dhidi ya Iran vinaashiria wazi kushindwa kwake kimkakati, kabla ya kuwa ni dhihirisho la nguvu za Marekani.