-
Kwa nini Marekani imeelekeza mashambulizi yake kusini mwa Iran?
Jul 16, 2026 07:27Hatua ya majeshi ya Iran ya kudhihirisha nguvu moja kupitia operesheni madhubuti kama vile kufunga Lango Bahari la Hormuz, inatoa ujumbe kwa adui kwamba hakuna migawanyiko yoyote iliyopo jeshini katika uwanja wa vita na kwamba uwezo wote wa taifa umejikita katika lengo moja la kulinda maslahi ya taifa kwa gharama yoyote ile, dhidi ya adui Mmarekani na Mzayuni.
-
Ni Argentina dhidi ya Uhispania, Waingereza wapigwa mweleka
Jul 16, 2026 06:24Lionel Messi na Argentina watacheza na Uhispania katika fainali ya Kombe la Dunia Jumapili ijayo baada ya kuifunga England mabao mawili katika dakika sita na sekunde 24 mwishoni mwa mechi kali ya nusu fainali na kuwavunja mioyo Waingereza.
-
Iran haina mipango ya kufanya mazungumzo, inalenga kujilinda: Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje
Jul 16, 2026 03:09Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema nchi hiyo haina mpango wa kurudi kwenye mazungumzo na Marekani maadamu Washington inaendelea kukiuka majukumu yake chini ya Mkataba wa Maelewano (MoU) uliosainiwa mwezi uliopita na nchi hizo mbili.
-
Waziri Mkuu wa Malaysia asema raia yeyote wa Israel atakayepatikana nchini huko atafukuzwa mara moja
Jul 16, 2026 03:07Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim, amesema Muisraeli yeyote atakaopatikana akiingia nchini humo atafukuzwa mara moja. Amesema hayo huku mamlaka za Malaysia zikichunguza ripoti kwamba Waisraeli walitumia hati mbili za kusafiria kuingia katika jimbo la kusini la Johor.
-
Umoja wa Mataifa waonya dhidi ya kutumia vibaya rasilimali za Sudan kufadhili vita
Jul 16, 2026 03:04Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba makundi yanayopigana nchini Sudan yanafaidika kutokana na udhibiti wa rasilimali za nchi hiyo, wakati uchumi wa vita ukichangia katika kuendeleza mzozo huo.
-
EU yaunga mkono ICC, yapinga kampeni ya Trump ya kuvunja mahakama ya uhalifu wa kivita
Jul 16, 2026 02:55Umoja wa Ulaya (EU) umesisitiza tena uungaji mkono wake kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), ukipinga kampeni mpya ya utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump ya kudhoofisha mahakama hiyo yenye makao yake makuu The Hague nchini Uholanzi.
-
Kofi Annan Foundation: Yumkini Kenya ikatumbukia katika ghasia za Uchaguzi Mkuu 2027
Jul 16, 2026 02:48Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi ya Kofi Annan Foundation imeonya kuwa nchi ya Kenya iko katika hatari kubwa ya kushuhudia vurugu zinazohusiana na uchaguzi mkuu wa 2027 iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.
-
Mkuu wa wakala bandia wa serikali ya Nigeria akamatwa baada ya kuwa mafichoni kwa wiki kadhaa
Jul 15, 2026 15:36Polisi ya Nigeria imemtia mbaroni mtu aliyeanzisha wakala bandia wa serikali uliokuwa ukifanyia kazi zake katika ofisi ya Rais kwa karibu miaka miwili.
-
UN yaonya: Tishio la kigaidi linaenea kote Afrika Magharibi na Sahel
Jul 15, 2026 12:06Umoja wa Mataifa umeonya kwamba makundi ya kigaidi yanapanua wigo wao kote Afrika Magharibi na Sahel, kwa kutumia mbinu za kisasa zaidi na kutishia amani ya majimbo ya pwani katika Ghuba ya Guinea.
-
UN yalaani mashambulizi dhidi ya wafanyakazi na miundombinu ya misaada ya kibinadamu nchini Iran
Jul 15, 2026 11:09Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) katika barua rasmi kwa Mkuu wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imelaani mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu, huduma za matibabu, magari ya wagonjwa na miundombinu ya misaada.