-
Iran yapinga madai ya Trump, yasema hakuna mazungumzo ya moja kwa moja yaliyofanyika na Marekani
Jul 15, 2026 10:07Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya kisheria na kimataifa, Kazem Gharibabadi, amepinga madai ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba Tehran na Washington zilifanya mazungumzo kwa saa 11, akisema hakuna mazungumzo yaliyofanyika Oman kati ya maafisa wa Iran na Marekani.
-
Pezeshkian: Tutalinda kila inchi ya ardhi ya Iran
Jul 15, 2026 09:18Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa kauli za maafisa wa Marekani na kusisitiza kwamba Iran italinda ardhi yake yote dhidi ya tishio la aina yoyote.
-
Kwa nini upinzani dhidi ya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran unaongezeka nchini Marekani?
Jul 15, 2026 06:27Mgogoro unaoendelea wa Marekani na Iran umefichua kwa uwazi zaidi kuliko huko nyuma, mipasuko ya kisiasa iliyopo huko Washington. Huku utawala wa Donald Trump ukisisitiza kuendeleza operesheni za kijeshi, upinzani unaongezeka bungeni, miongoni mwa umma kwa ujumla, na hata miongoni mwa baadhi ya Warepublican.
-
Bunge la Iran lawasilisha muswada wa kusimamia Lango Bahari la Hormuz
Jul 15, 2026 03:59Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limewasilisha rasmi muswada wa sheria unaolenga kuimarisha usimamizi wa Mlango Bahari wa Hormuz, hatua inayokuja wakati wa kuongezeka kwa mvutano na uingiliaji wa Marekani katika njia hiyo muhimu ya kimkakati ya baharini.
-
Uhispania yaibamiza Ufaransa na kutinga fainali ya Kombe la Dunia
Jul 15, 2026 03:57Timu ya taifa ya soka ya Uhispania imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Dunia la Fifa 2026 baada ya kuilaza Ufaransa kwa ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa mjini Dallas, Marekani.
-
Iran: Uamuzi wa Uingereza kuhusu jeshi la Sepah unakiuka sheria za kimataifa
Jul 15, 2026 03:53Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekemea vikali uamuzi wa serikali ya Uingereza wa kulitaja Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kuwa ni “tishio chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa ya Uingereza,” ikisema hatua hiyo “haina msingi na isiyo ya uwajibikaji” na inakiuka sheria za kimataifa.
-
Oman: Tishio hatari zaidi halitokani na Tehran bali Tel Aviv
Jul 15, 2026 03:52Serikali ya Oman imesema tishio kubwa zaidi kwa usalama na utulivu wa eneo halitokani na Tehran, bali linatoka Tel Aviv.
-
Lavrov: Kuanza tena mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran ni ukiukaji wa Makubaliano
Jul 15, 2026 03:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov, amesema kuwa kuanza tena mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran ni ukiukaji wa Hati ya Makubaliano (MoU) iliyotiwa saini kati ya Tehran na Washington.
-
Jeshi la Iran kwa Marekani: Lango la Hormuz halitafunguliwa kamwe kupitia vita na uchokozi
Jul 14, 2026 11:14Msemaji wa Jeshi la Iran ametoa onyo kali kwa Marekani kuwa hakuna kitendo chochote cha uchokozi kitakachoweza kulazimisha kufunguliwa kwa Lango la Bahari la Hormuz, kufuatia uamuzi wa Tehran wa kulifunga lango hilo la kimkakati baada ya Marekani kukiuka makubaliano.
-
Iran yawasilisha malalamiko rasmi UN kuhusu ukiukaji wa Marekani wa Mkataba wa Islamabad
Jul 14, 2026 11:12Iran imewasilisha rasmi malalamiko ya kina kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC), ikilaani vikali Marekani kwa kukiuka kwa mfumo Mkataba wa Maelewano (MoU) wa Islamabad uliotiwa saini mwezi uliopita.