-
Iran: Uamuzi wa Uingereza kuhusu jeshi la Sepah unakiuka sheria za kimataifa
Jul 15, 2026 03:53Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekemea vikali uamuzi wa serikali ya Uingereza wa kulitaja Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kuwa ni “tishio chini ya Sheria ya Usalama wa Taifa ya Uingereza,” ikisema hatua hiyo “haina msingi na isiyo ya uwajibikaji” na inakiuka sheria za kimataifa.
-
Oman: Tishio hatari zaidi halitokani na Tehran bali Tel Aviv
Jul 15, 2026 03:52Serikali ya Oman imesema tishio kubwa zaidi kwa usalama na utulivu wa eneo halitokani na Tehran, bali linatoka Tel Aviv.
-
Lavrov: Kuanza tena mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran ni ukiukaji wa Makubaliano
Jul 15, 2026 03:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov, amesema kuwa kuanza tena mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran ni ukiukaji wa Hati ya Makubaliano (MoU) iliyotiwa saini kati ya Tehran na Washington.
-
Jeshi la Iran kwa Marekani: Lango la Hormuz halitafunguliwa kamwe kupitia vita na uchokozi
Jul 14, 2026 11:14Msemaji wa Jeshi la Iran ametoa onyo kali kwa Marekani kuwa hakuna kitendo chochote cha uchokozi kitakachoweza kulazimisha kufunguliwa kwa Lango la Bahari la Hormuz, kufuatia uamuzi wa Tehran wa kulifunga lango hilo la kimkakati baada ya Marekani kukiuka makubaliano.
-
Iran yawasilisha malalamiko rasmi UN kuhusu ukiukaji wa Marekani wa Mkataba wa Islamabad
Jul 14, 2026 11:12Iran imewasilisha rasmi malalamiko ya kina kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC), ikilaani vikali Marekani kwa kukiuka kwa mfumo Mkataba wa Maelewano (MoU) wa Islamabad uliotiwa saini mwezi uliopita.
-
Wanachama wawili wa kundi la kigaidi la Daesh wanyongwa nchini Iran
Jul 14, 2026 11:10Wanachama wawili wa kundi la kigaidi la wakufurishaji la Daesh (ISIS), ambao walipatikana na hatia ya kupanga kutekeleza vitendo vya kigaidi na uasi wa kutumia silaha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, wamehukumiwa kifo na kunyongwa baada ya hukumu zao kuthibitishwa na Mahakama Kuu ya Iran.
-
Jeshi la Sudan lakomboa eneo la Fashfoun katika jimbo la Blue Nile baada ya mapigano na waasi
Jul 14, 2026 11:03Jeshi la Sudan limesema mapema Jumanne kuwa limekomboa eneo la Fashfoun katika jimbo la Blue Nile baada ya mapigano na waasi wa makundi ya RSF na SPLM-N.
-
Kwa nini Makubaliano ya Islamabad yamekumbwa na mgogoro?
Jul 14, 2026 11:02Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea hatua za kichokozi za utawala wa Marekani kuwa ni ukiukaji wa makubaliano ya Islamabad na chanzo cha mgogoro unaohusu utekelezaji wake.
-
UN: Msaada wa haraka wahitajika Somalia kukabiliana na ukame mkali
Jul 14, 2026 11:01Shirika la misaada la Umoja wa Mataifa (UN) limetoa wito wa msaada wa dharura kwa mamia ya maelfu ya watu wa Somalia, hasa katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo, ambao wanakabiliwa na hali ngumu inayozidi kuongezeka kutokana na ukame mkali.
-
Iran: Mkataba wa Islamabad umevurugwa na Marekani
Jul 14, 2026 04:48Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa mkataba wa maelewano (MoU) uliosainiwa hivi karibuni baina yake na Marekani sasa uko katika hali ya mkwamo, kufuatia hatua ya Washington kukiuka ahadi zake. Mkatataba huo unajulikana kama Mkataba wa Islamabad kutokana na kuhusika Pakistan katika jitihada za upatanishi baina ya pande hizo mbili.