Tehran yaikosoa Magharibi kwa kutoweza kutatua migogoro inayojitengenezea yenyewe
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i138422-tehran_yaikosoa_magharibi_kwa_kutoweza_kutatua_migogoro_inayojitengenezea_yenyewe
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amemsihi mwandishi anayepinga ukoloni, Aimé Césaire, kulaani uozo wa maadili, unafiki na kushindwa kwa nchi za Magharibi kukabiliana na migogoro iliyotokana na vita na udhibiti wao.
(last modified 2026-05-17T02:49:53+00:00 )
May 17, 2026 02:45 UTC
  • Esmaeil Baqaei
    Esmaeil Baqaei

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amemsihi mwandishi anayepinga ukoloni, Aimé Césaire, kulaani uozo wa maadili, unafiki na kushindwa kwa nchi za Magharibi kukabiliana na migogoro iliyotokana na vita na udhibiti wao.

Esmaeil Baqaei alitoa maoni hayo katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X jana Jumamosi, akinukuu kutoka kwenye makala ya Césaire, "Majadiliano Kuhusu Ukoloni" (Discourse on Colonialism) ya mwaka 1950.

"Ustaarabu ambao hauwezi kutatua matatizo unayoyatengeneza wenyewe ni ustaarabu uliooza; ustaarabu unaochagua kufumbia macho matatizo yake muhimu zaidi ni ustaarabu mgonjwa," ameandika Ismael Baqaei.

Pia amenukuu onyo la Césaire kwamba tawala zilizojengwa juu ya unafiki hatimaye hupoteza uwezo wa kudanganya ulimwengu.

"Ustaarabu unaochezea misingi na kanuni zake ni ustaarabu unaokufa," amesema Baqaei na kuongeza: Unakimbilia katika unafiki ambao ni mbaya zaidi kwa sababu kuna uwezekano mdogo wa kudanganya."

Matamshi hayo yametolewa huku Marekani na Israel zikiendelea kupiga ngoma za vita dhidi ya Iran jambo ambalo limefichua mgawanyiko unaoongezeka ndani ya muungano wa Magharibi na kuzidisha misukosuko ya kiuchumi kote duniani.

Sasa, kile ambacho Washington na Tel Aviv zilikielezea hapo awali kama vita vya kuiangamiza Iran na kuilazimisha kusalimu amri kisiasa kimebadilika na kuwa mapambano ya kikanda yenye gharama kubwa bila ushindi dhahiri kwa madola hayo mawili ya kibeberu.