Jeffrey Sachs: Walioishambulia Iran wanapasa kuarifishwa kama pande zilizoshindwa vitani
-
Jeffrey Sachs
Mchumi mashuhuri wa Marekani, anaamini kuwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa, walioanzisha mashambulizi dhidi ya Iran wanapaswa kuarifishwa kama pande zilizoshindwa vitani; wamekiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa na wanawajibika kwa uharibifu na matokeo ya vita walivyovianzisha.
Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, Jeffrey Sachs, mchumi na mchambuzi mashuhuri wa Marekani, amechunguza chanzo cha mvutano kati ya Iran, Israel na Marekani katika mahojiano na Shirika la Habari la IRNA na kuwasilisha simulizi tofauti ya matukio ya hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi kwa mujibu wa sheria za kimataifa na hali ya kijiopolitiki.
Amekosoa siasa za Marekani na Israel na kutilia shaka madai yanayotolewa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. Sachs anaamini kuwa, vita vya hivi karibuni si tu kwamba vilishindwa kufikia malengo yaliyotangazwa ya Washington na Tel Aviv, bali pia vimezidisha ukosefu wa amani katika Asia Magharibi na kuathiri uchumi wa dunia.
Jeffrey Sachs ni mchumi mtajika wa Marekani na Profesa katika Chuo Kikuu cha Columbia, na mmoja wa wachambuzi mashuhuri wa maendeleo endelevu na uchumi wa dunia. Amekuwa mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo na kupunguza umaskini duniani, na amewasilisha mitazamo yenye ushawishi juu ya mada kama vile uchumi wa kimataifa, mabadiliko ya hali ya tabia nchi na sera ya kigeni za Marekani.
Tangu mwanzoni mwa miaka ya tisini, Netanyahu amekuwa akidai kuwa Iran iko karibu sana kuunda bomu la nyuklia. Amekuwa akitoa madai haya yasiyo msingi kwa zaidi ya miaka 30 sasa.