Mar 03, 2024 04:37 UTC
  • Yemen: Operesheni katika bahari Nyekundu zinaendelea

Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen imesisitiza udharura wa kuendelezwa operesheni za vikosi vya majini vya nchi hiyo hadi hapo utawala wa Kizayuni wa Israel utakapositisha jinai zake huko Ukanda wa Gaza.

Katika miezi ya karibuni jeshi la Yemen limekuwa likizishambulia meli za utawala wa Kizayuni wa Israel au zile zinazoelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina katika kuunga mkono mapambano ya ukombozi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza. Jeshi la Yemen linatekeleza mashambulizi hayo katika Bahari Nyekundi na katika mlango bahari wa Bab el Mandab. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Yemen imeeleza kuwa, utawala ghasibu wa Israel na waitifaki wake wanahusika katika hali ya mvutano inayoshtadi katika Bahari Nyekundu na katika mlango bahari wa Bab el Mandab. 

Katika upande mwingine, Shirika la Biashara ya Baharini la Uingereza jana lilitangaza kuwa limepokea ripoti ya kujiri shambulio la baharini umbali wa maili 15 magharibi mwa bandari ya Mokha huko Yemen. 

Vyombo vya habari vya Kiarabu pia vimeripoti kuwa, shambulio hilo lilitekelezwa masaa kadhaa baada ya kuzama meli ya mizigo ya Uingereza M/V Rubymar, katika bahari Nyekundu. Meli hiyo ambayo ilikuwa imepakia  tani 41,000 za mbolea, ilishambuliwa na jeshi la Yemen katika Bahari Nyekundu siku 14 zilizopita yaani Februari 18 mwaka huu. 

Meli ya mizigo ya Uingereza iliyozama bahari katika Nyekundu 

Harakati ya Ansarullah ya Yemen kwa mara nyingine tena jana ilitangaza kuwa itaruhusu meli ya Uingereza iliyozama kuondolewaka katika Bahari Nyekundu pale misaada ya kibinadamu itakaporuhusiwa kuingia  Ukanda wa Gaza.

Tags