Apr 03, 2023 11:50 UTC
  • Polisi wa kike wasimamia ibada ya Hija na Umra kwa mara ya kwanza nchini Saudi Arabia

Kwa mara ya kwanza nchini Saudi Arabia, doria za polisi zinafanyika katika ibada ya Hija na Umra kwenye mwezi wa Ramadhani kwa kushirikisha askari usalama wa kike.

Kwa mujibu wa tovuti ya Al-Hurra, mkanda wa video uliosambazwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, unawaonyesha askari usalama wa kike wakishirikiana na wenzao wanaume kusimamia mahujaji wa ibada ya Umrah na kuwaongoza katika safu za Swala na twawafu kandokando Nyumba ya Mwenyezi Mungu, al Kaaba.

Vyombo vya usalama vya Saudia vimetangaza kwamba: Kuwepo kwa skari wanawake katika shuguli ya kusimamia ibada ya Umra kwa hakika kunafanyika katika mwendelezo wa kazi ya muundo jumuishi wa usalama kwa ajili ya kudumisha amani na kulinda afya za mahujaji wa Msikiti wa Al-Haram.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumeanza kufanyika mageuzi nchini Saudi Arabia, ikiwa ni pamoja na kupunguzwa vizuizi vilivyowekwa kwa wanawake wa Saudia, kama vile kuwaruhusu kuendesha gari mnamo hapo 2018, ukuzaji wa soko la ajira kwa wanawake, kuwaruhusu kusafiri nje ya nchi biya ya mahramu na kuwaruhusu kufanya kazi katika sekta ambazo hapo awali zilikuwa makhsusi kwa wanaume.

Image Caption

Vilevile Wizara ya Hija na Umra ya Saudia mwezi uliopita iliwaruhusu wanawake kutekeleza ibada ya Hija bila mahramu, ili mradi wawe katika kundi la wanawake wengine.

Tags