-
Wananchi wa Uganda walalamikia ziara ya Netanyahu nchini mwao
Jul 05, 2016 02:44Raia nchini Uganda wamekosoa ziara ya Waziri Mkuu wa Utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu nchini humo, kutokana na ukatili wa kutisha unaofanywa na utawala huo dhidi ya wananchi madhlum wa Palestina. Waganda wameihoji serikali yao kwa kumwalika Netanyahu huku akijua kuwa kiongozi huyo wa Israel ni mvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu.
-
Utamu wa kabumbu... Pasi za ajabu katika kandanda... Utafurahi
Jul 04, 2016 04:41Kila mchezo una mvuto wake, lakini kwa mashabiki wa kandanda, watakubaliana nami kuwa, mvuto ulioomo kwenye kipande hiki cha video hawajawahi kuona mfano wake... Pasi ipi imekuvutia zaidi? Nina yakini utashindwa kujua ipi imekumaliza zaidi... Ajabu ni kuwa pasi hizo zimetolewa kwenye michuano migumu, si katika mazoezi...
-
Vijana wa Lamu Kenya wafanya usafi kujitayarisha kwa sikukuu ya Idul Fitr
Jul 02, 2016 08:21Vijana wa Lamu nchini Kenya wameendeleza sunna nzuri ya kufanya usafi kwa ajili ya kujitayarisha kwa sikukuu kubwa ya Waislamu, sikukuu ya Idul Fitr. Video hii inaonesha baadhi ya vijana hao wakiwa kazini wakizungumzia suala hilo...
-
Baadhi ya wakati wanyama wanawazidi binadamu kwa kuoneana huruma
Jul 02, 2016 05:35Baadhi ya wakati wanyama huoneana huruma kuliko hata wanadamu, kama wanavyoonesha makobe hawa wawili katika kipande hiki cha video kilichoenea kwenye mitandao ya kijamii.
-
Mchezo mwingine wa kucheza na roho za watu haufai...
Jul 02, 2016 05:27Rubani wa ndege hii, bila ya kujali idadi kubwa ya roho za watu zilizoko kwenye dhima yake, alifanya mchezo huu wakati akirusha ndege. Michezo ya namna hii haifai...
-
Jeshi la Iraq liliposhambulia msafara mkubwa wa Daesh nje ya Fallujah
Jul 02, 2016 04:40Baada ya kuzidiwa nguvu katika mji muhimu na wa kiistratijia wa Fallujah nchini Iraq, kundi la Daesh (ISIS) liliamua kukimbia kwenye msafara mkubwa wa magari kuelekea upande wa Syria kwa ajili ya kuunganisha nguvu upya. Hata hivyo jeshi la anga la Iraq liliushambulia vikali msafara huo wa Daesh kama inavyoonesha video hii kutoka Wizara ya Ulinzi ya Iraq.
-
Basi la shule
Jun 28, 2016 01:51Duniani kuna maajabu, hili ni moja ya maajabu hayo...
-
Subhanallah! Mtu anavyojitahidi kumwokoa papa baharini
Jun 28, 2016 01:47Kipande hiki cha video kimeenea katika mitandao ya kijamii kikimuonesha mtu akijaribu kadiri awezavyo kumuokoa papa "aliyepwewa" baharini. Ajabu ni kuwa kadiri papa alivyokuwa anarudishwa baharini, alikuwa ndio kwanza anarejea nchi kavu...
-
Yaliyomsibu mvuvi
Jun 28, 2016 01:43Yaliyomsibu mvuvi aliyetaka kuvua samaki mkubwa kwa hali yoyote ile. Pamoja na tabu na madhara na mashaka, hatimaye...
-
Unyanyasaji wa Wazayuni na mateso ya Wapalestina
Jun 25, 2016 07:03Ijumaa ya wiki hii ni Siku ya Kimataifa ya Quds. Tumekuwekea kipande hiki cha video kinachoonesha namna wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanavyowatesa Wapalestina katika ardhi yao wenyewe...