-
Waislamu Kenya watakiwa kutofuata mwezi wa Saudia bali kufuata mwandamo wa kwao + Sauti
Aug 22, 2018 13:28Waislamu nchini Kenya wametakiwa kuzingatia mwezi mwandamo katika ukanda wa Afrika Mashariki ili kufanikisha maamuzi ya kiibada kama vile funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, Idul Fitr na Idul Adh'ha na kuacha kufuata Saudi Arabia au mwezi wa kimataifa. Seifullah Murtadha ametuandalia ripoti maalumu kuhusu suala hilo...
-
Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu 1439 Hijria + Sauti
Aug 20, 2018 04:15Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika ujumbe wake uliosomwa leo kwa Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwamba sera za Marekani ni kuchochea vita baina ya Waislamu na akasisitiza kwamba: inapasa kuzizima sera hizo za kishetani kwa umakini na kuwa macho na kwamba Hija na kujibari na washirikina vinawezesha kupatikana umakini huo.
-
SAUTI, Sheikh Jalala: Nchi zilizowakoloni Waafrika zilipe fidia kwa nchi za bara hilo, sambamba na kutupiliwa mbali mitaala yao
Aug 17, 2018 11:43Kiongozi wa Chuo cha Imam Swadiq (as) cha jijini Dar es Salaam, Tanzania Sheikh Hemed Jalala, ameonya tabia ya nchi za Kiafrika kuendelea kukumbatia mitaala na maelekezo ya nchi za kikoloni na kibeberu kwa kuwa mabeberu hao hawana nia njema na bara la Afrika.
-
Sauti, Serikali ya Cameroon yakasirishwa na kusambaa video zinazowaonyesha askari wakiwatesa raia na kuwamiminia risasi
Aug 17, 2018 11:42Serikali ya Cameroon imesema kuwa, haitoifumbia macho mikanda ya video inayoenezwa katika mitandao ya kijamii ikiwaonyesha askari wa nchi hiyo wakiwanyanyasa na kuwaua wananchi.
-
SAUTI, Waziri wa Sheria na Katiba Tanzania: Serikali imeamua kuyaweka mashirika yote ya umma chini ya Mwanasheria Mkuu
Aug 16, 2018 11:07Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi amesema, serikali imeamua kuyaweka mashirika yote ya umma kuanzia Tanesco, mifuko ya hifadhi ya jamii na bandari chini ya usimamizi wa Mwanasheria Mkuu wa serikali kwa lengo la kuzuia mashirika hayo kuendelea kupata hasara.
-
Kinyang'anyiro cha ubunge chaingia kasi nchini Rwanda
Aug 16, 2018 03:36Nchini Rwanda, kampeni za ubunge za kuwania viti vya uwakilishi bungeni katika uchaguzi wa uliopangwa kufanyika mwezi ujao wa Septemba zinaendelea.
-
Wabunge Uganda wachachamaa, wataka kujua hatima ya wenzao waliokamatwa na polisi
Aug 16, 2018 03:28Spika wa Bunge la Uganda, Jumatano alilazimika kusimamisha vikao vya bunge kwa muda wa saa moja baada ya kuombwa na wabunge waende wakafuatilie hatima ya wabunge wenzao waliowekwa kizuizini na polisi. Kigozi Ismail ametuandalia ripoti maalumu kuhusu habari hiyo...
-
SAUTI, UN yamtaja Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kuwa kiongozi pekee barani Afrika anayepambana na ufisadi
Aug 14, 2018 11:46Umoja wa Mataifa umempongeza Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kutokana na juhudi kubwa za kupambana na ufisadi anazozitekeleza nchini humo.
-
Upinzani wazidi kupata pigo Tanzania, Mtatiro naye ahamia CCM + SAUTI
Aug 11, 2018 10:28Mrengo wa upinzani nchini Tanzania umeendelea kupata pigo kutokana na viongozi wake mashuhuri kuhamia chama tawala cha Mapinduzi CCM baada ya Julius Mtatiro, Mwenyekiti wa Chama cha CUF kambi ya Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza leo kwamba, amekihama chama hicho na kuhamia CCM.
-
SAUTI, Mufti wa Zanzibar Sheikh Omar Al Kaabi, awataka Waislamu kutoichezea ndoa ya Kiislamu.
Aug 10, 2018 12:03Mufti wa Zanzibar Saleh Omar Al Kaabi, amewataka Waislamu kuheshimu na kuienzi ndoa kwa ajili ya kujenga jamii bora yenye kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu.