-
SAUTI: Waasi wa Ninja nchini Congo-Brazzaville wazidi kuwa tishio, waua askari wengi na kuteka mabasi ya abiria
May 27, 2017 10:48Kitendo cha Waasi wa Ninja nchini Congo Brazzaville kuteka mabasi mawili ya abiria katika misitu ya nchi hiyo, kimelifanya jeshi kupatwa na wasi wasi na kutuma helikopta za kijeshi kwa lengo la kuwaokoa watu hao.
-
SAUTI: Waislamu Kenya: Serikali ya Jubilee isitumie suala la uhuru wa Ramadhani katika kampeni, ni haki ya kila Mkenya
May 23, 2017 13:32Shakhsia mbalimbali wa Kiislamu nchini Kenya, wameitaka serikali kuwahakikishia Waislamu usalama wa kutosha ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani baada ya serikali hiyo kuondoa hali ya hatari katika maeneo ya mpakani na Somalia.
-
SAUTI: Polisi ya Kinshasa yawabembeleza wakazi wa mji huo kuwataja wafungwa waliotoroka jela kuu, nao uvamizi wa jela wakikithiri
May 19, 2017 13:41Polisi ya mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewataka wakazi wa mji huo kuisaidia serikali katika kuwataja wafungwa waliotoka jela kuu ya jiji hilo.
-
SAUTI: Viongozi wa chama cha UDPS Kongo DR wawekwa kizuizini na polisi siku tatu, kuwazuia kujadili kuurejesha mwili wa Tshisekedi
May 13, 2017 14:07Huku mgogoro juu ya suala la kusafirishwa, kuagawa na kuzikwa kwa mwili wa mzee Étienne Tshisekedi kiongozi wa upinzani wa chama cha The Union for Democracy and Social Progress huko Kongo DR, ukiendelea kutokota, jeshi la polisi limewaweka kizuizini kwa siku tatu viongozi wa chama hicho.
-
SAUTI: Kadhia ya kusafirishwa, kuagwa na hatimaye kuzikwa mwili wa mzee Étienne Tshisekedi wa Kongo DR, bado kitendawili
May 12, 2017 12:36Suala la kusafirishwa, kuagwa na hatimaye kuzikwa mwili wa mzee Étienne Tshisekedi kiongozi wa upinzani wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, limeendelea kuwa kitendawili baada ya upande wa serikali na upinzani kushindwa kuafikiana kuhusiana na suala hilo.
-
SAUTI: Kongamano la viongozi wa Afrika la Sayansi na Teknolojia lamemalizika Kigali, Rwanda bila kufikiwa makubaliano
May 12, 2017 12:31Kongamano la siku tatu lililokuwa likifanyika mjini Kigali, Rwanda kuhusiana na masuala ya sayansi na teknolojia limemalizika bila kufikiwa makubaliano tarajiwa.
-
SAUTI: Uhaba wa fuel nchini Burundi umeendelea kushuhudiwa, licha ya juhudi za serikali ya nchi hiyo kufanyika bila mafanikio
May 09, 2017 12:52Na nchini Burundi uhaba wa fuel kwa ajili ya vyombo vya usafiri umeendelea kushuhudiwa licha ya serikali ya Bujumbura kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kupitisha sharia mpya za ugavi wa nishati hiyo.
-
SAUTI: Viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika wakamilisha kikao chao mjini Kigali Rwanda na ajenda ya 'kuchapa kazi na kuachana na maneno'
May 08, 2017 12:17Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za bara la Afrika wamekamilisha kikao chao cha faragha kilichodumu kwa siku mbili mjini Kigali, Rwanda.
-
SAUTI: Waandishi Burundi walalamikia wanavyobanwa, mazingira hatari na ukosefu wa usalama kazini
May 04, 2017 13:34Mkuu wa kituo cha waandishi habari nchini Burundi amesema, maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari yanafanyika wakati waandishi nchini humo wakifanya kazi katika hali ya woga kiasi kwamba katika kipindi cha miaka miwili ya mzozo wa nchi hiyo uhuru wa vyombo vya habari umebakia katika maandishi na si katika vitendo. Maelezo zaidi na mwandishi wa Bujumbura, Hamida Issa...
-
SAUTI: Wimbi la kushambuliwa raia wa Kenya waliojitoa kwenye kundi la kigaidi la al Shabab
May 03, 2017 13:46Familia zilizo na ufahamu wa watoto wao kujiunga na harakati za kundi la kigaidi la al-Shabab nchini Somalia zimetakiwa kujitokeza na kutoa ripoti kwa vyombo vya usalama ya Kenya.