-
UN: Watu milioni 500 hawana usalama wa maji barani Afrika
Mar 22, 2022 01:58Umoja wa Mataifa umesema watu zaidi ya milioni 500 katika nchi 19 za bara Afrika wanasumbuliwa na ukosefu wa maji safi na salama.
-
Sierra Leone: Si haki Afrika kutowakilishwa katika Baraza la Usalama la UN
Mar 13, 2022 04:30Waziri wa Mambo ya Nje wa Sierra Leone ametoa mwito wa kupewa nchi ya Kiafrika uanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Kwa akali watu 17 wauawa katika mapigano ya makundi hasimu Darfur, Sudan
Mar 11, 2022 20:33Kwa akali watu 17 wameuawa huko Darfur magharibi mwa Sudan baada ya kuibuka mapigano baina ya makundi mawili hasimu.
-
Afrika Kusini yataka Afrika itumie sarafu moja itakayoimarisha biashara
Mar 11, 2022 04:41Afrika Kusini imesema inaunga mkono wazo la kuanzisha sarafu moja ambayo itapiga jeki miamala ya kibiashara miongoni mwa nchi za bara hilo.
-
Karibu watoto milioni tatu kupata chanjo ya polio Malawi
Mar 04, 2022 23:23Madaktari na wauguzi watatoa chanjo za kujikinga na ugonjwa wa polio kwa watoto wasiopungua milioni 2.9 huko Malawi. Hayo yameelezwa na Umoja wa Mataifa baada ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu kuugua ugonjwa huo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Lilongwe.
-
Rais wa Guinea-Bissau: Kinara wa dawa za kulevya amehusika na mapinduzi yaliyofeli
Feb 11, 2022 23:27Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embalo, amemshutumu mkuu wa zamani wa jeshi la wanamaji anayehusishwa na biashara ya dawa za kulevya na washirika wake wawili kuwa walihusika na mapinduzi yaliyoshindwa mapema mwezi huu.
-
WHO: Kesi za Corona Afrika ni mara saba zaidi ya ilivyoripotiwa
Feb 10, 2022 23:01Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kesi za maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika ni mara saba zaidi ya kesi zilizoripotiwa rasmi kufikia sasa katika nchi za bara hilo.
-
Tahadhari ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali mbaya eneo la Pembe ya Afrika
Feb 09, 2022 23:27Huku mizozo ya kisiasa na kijamii ikiendelea katika ukanda wa Afrika Mashariki, nchi nyingi za kanda hiyo zinakabiliwa na ukame mkubwa; na ambamba na hayo Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza kuwa ukame umesababisha takriban watu milioni 13 katika Pembe ya Afrika kukumbwa na njaa.
-
WFP: Mamilioni wanakabiliwa na njaa Pembe ya Afrika
Feb 08, 2022 09:21Watu wanaokadiriwa kuwa milioni 13 katika eneo la Pembe ya Afrika wanakabiliwa na njaa kali. Hayo yameelezwa leo Jumanne na Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP).
-
Wapalestina wautaka Umoja wa Afrika kuifukuza Israel katika umoja huo
Feb 05, 2022 10:47Viongozi na makundi ya ukombozi wa Palestina wameutaka Umoja wa Afrika (AU) kufikiria upya uamuzi wa mwaka jana wa kuipa Israel hadhi ya kuwa mwangalizi katika umoja huo.