Nchi za Afrika Magharibi zakubaliana kuhusu mkakati wa hali ya hewa
Viongozi wa Jumuiya ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) wamekubaliana kuhusu stratijia ya kikanda kwa ajili ya kushughulikia ongezeko la joto duniani katika kipindi cha miaka kumi ijayo.
Katika makubaliano yao na Umoja wa Ulaya (EU), nchi wanachama wa jumuiya ya ECOWAS zimepanga kutumia dola bilioni 294 katika miaka kumi ijayo ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.
Sekou Sangare Kamishna wa jumuiya ya ECOAWS anayehusika na masuala ya kilimo, mazingira, na vyanzo vya maji amesema kuwa,walikadiria matumizi ya lazima kati ya mwaka 2020 na 2030 kugharimu dola zisizopungua 294.
Vile vile amesema, stratejia hiyo pia imekusudia kuzidisha kiwango cha ufahamu kuhusu kupitisha mitindo mipya ya maisha ili kusaidia kupatia ufumbuzi ongezeko la joto duniani. Stratejia hiyo ya kikanda ya nchi za Magharibi mwa Afrika kwa ajili ya kushughulikia ongezeko la joto duniani.
Amesisitiza pia kuwa, ECOWAS inataka kuwepo ushirikiano baina ya taasisi za kieneo, baina ya nchi 15 wanachama wa Ecowas, washirika wao na washika dau wa taasisi za kijamii za kieneo na kimataifa.
Jumuiya ya Ecowas iliongoza mchakato huo mwaka 2020 kupitia mkakati uliofadhiliwa na Umoja wa Ulaya.
Karibu asilimia 56 ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Benin, Cote D'voire yaani Ivory Coast, Senegal na Togo yameathiriwa na mmomonyoko wa ardhi; athari ambazo zinatazamiwa kuongezeka.