Waafrika wazidi kuonesha ubinadamu, wampa tunzo maalumu Yahya Sinwar
Waafrika kwa mara nyingine wameonesha hisia zao za kuthamini ubinadamu kwa kuenzi nafasi muhimu ya wanamapambano wa Palestina. Tuzo ya ya kila mwaka ya "Kwame Tour" kwa mwaka huu 2025 amepewa kiongozi wa Palestina shujaa shahid Yahya Sinwar (Abu Ibrahim) wakati wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Afrika.
Shahid Yahya Sinwar, Mkuu wa zamani wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, aliuliwa kigaidi na Israel kwenye Ukanda wa Ghaza mwaka 2024.
Katika hafla ya kuonesha kuenzi na kuheshimu mapambano ya kimataifa dhidi ya ukoloni na ukandamizaji, Chama cha Revolutionary Pan-African Peoples’ kimeipa familia ya Yahya Sinwar (Abu Ibrahim) Tuzo yake ya Kwame Tour ya mwaka huu wa 2025.
Hatua hiyo imechukuliwa kutambua na kuenzi nafasi yake ya kwanza katika kuongoza Muqawama wa Palestina na mapambano ya haki na ya kishujaa ya Wapalestina dhidi ya uvamizi wa Israel.
Sherehe za kukabidhiwa tunzo hiyo ziliambatana na kumbukumbu ya Siku ya Uhuru wa Afrika - inayoadhimishwa tareheh 25 Mei kila mwaka. Sherehe hizo zinafanyika kwa mnasawa kuasisiwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika OAU ulioanzishwa mwaka 1963. Hivi sasa OAU imebadilishwa jina na kuwa Umoja wa Afrika yaani AU. Waafrika wanaheshimu sana mapambano ya ukombozi wa Palestina katika kipindi chote hiki.
Siku chache zilizopita Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola Tete Antonio alisema kuwa, Umoja wa Afrika (AU) hauwezi kuwa na furaha unapoona kuna njama za kuwapora Wapalestina ardhi zao na kutaka kuwapeleka barani Afrika.
Akiwakilishi bara zima la Afrika, Waziri Antonio alisema hayo mbele ya waandishi wa habari akiwa pamoja na mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, baada ya kumalizika mkutano wa tatu wa mawaziri wa EU-AU mjini Brussels na kuongeza kuwa, “Msimamo wa AU wa kuwaunga mkono Wapalestina na watu wanaodhulumiwa utaendelea kuwa vilevile.”
Alisema: Mgeni pekee mwalikwa wa kudumu wa AU katika mikutano yake ya kilele alikuwa ni Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, akiongeza kuwa jambo hilo linaonesha msimamo wa AU kuhusu Palestina.