Mapigano na mashambulio ya makundi ya wabeba silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yangali yanaendelea kushuhudiwa.
Mwakilishi wa mji wa Bocaranga, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameitaka serikali ya nchi hiyo kudhamini usalama wa eneo hilo la mpakani kutokana na hujuma za makundi ya wabeba silaha.
Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza kuwa, kwa akali watu 15 wameuawa katika shambulizi la makundi ya wabeba silaha katika mji wa Bukaranga uliopo kaskazini mwa nchi hiyo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kuwa kama litaendelea kukabiliwa na matatizo litalazimika kusimamisha upelekaji misaada kwa maelfu ya wakimbizi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Rais Faustin Archang Touadera wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kufungamana na kuwa karimu zaidi katika kuboresha hali ya kiuchumi ya nchi yake.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ametoa wito wa kuwepo mshikamamo na ukarimu wa jamii ya kimataifa kwa nchi yake ili kusaidia kuboresha hali ya mambo nchini humo.
Watu 11 wameuawa katika shambulio la watu wenye silaha kwenye kambi ya wakimbizi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Askari jeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa waliopo Jamhuri ya Afrika ya Kati wametangaza kutiwa mbaroni mamluki kadhaa wa kundi moja lenye silaha nchini humo.
Jeshi la Uganda limechukua uamuzi wa kuondoa wanajeshi wake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kusaidia jitihada za kuwaangamiza waasi wa Uganda.
Taasisi za kimataifa zimekaribisha hatua ya kuidhinishwa Rais mpya wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.