Jun 29, 2016 07:19 UTC
  • Jeshi la Uganda laamua kuondoa vikosi vyake CAR

Jeshi la Uganda limechukua uamuzi wa kuondoa wanajeshi wake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kusaidia jitihada za kuwaangamiza waasi wa Uganda.

Kanali wa Pili Paddy Ankunda ambaye ni Msemaji wa jeshi la Uganda amesema kuwa jeshi la nchi hiyo jana lilichukua uamuzi wa kuondoa wanajeshi wake 2500 walioko Jamhuri ya Afrika ya Kati kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba ili kuweza kushirikiana na nchi nyingine za eneo katika kuwaangamiza waasi wa Uganda wa LRA chini ya Uwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).

Kanali wa Pili Paddy Ankunda ameongeza kuwa waasi wa Uganda wa Jeshi la Kikristo (LRA) wamedhoofika pakubwa na kwamba hawana uwezo wa kufanya mashambulizi ya utumiaji silaha.

Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika mwezi uliopita liliitaka serikali ya Uganda itazame upya uamuzi wake wa kutaka kuondoa wanajeshi wake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa sababu hatua kama hiyo itasababisha ombwe la kiusalama na kuzidisha hujuma za waasi wa LRA na makundi mengine ya waasi.

Tags