Nov 17, 2016 15:53 UTC
  • Jamhuri ya Afrika ya Kati yaomba msaada kuboresha hali ya nchi

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ametoa wito wa kuwepo mshikamamo na ukarimu wa jamii ya kimataifa kwa nchi yake ili kusaidia kuboresha hali ya mambo nchini humo.

Rais Faustin-Archange Touadera wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameyasema hayo leo wakati wa kuanza mkutano wa nchi wafadhili huko Brussels Ubelgiji. Ameiomba jamii ya kimataifa isaidie kuboresha hali ya kiuchumi ya nchi hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati pia ametangaza mpango wa maendeleo ya kiuchumi kwa ajili ya nchi yake wenye thamani ya dola bilioni tatu na milioni mia moja katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2017 hadi 2021.

Baadhi ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliolazimika kuyahama makazi yao kutokana na mapigano

Ameongeza kuwa, dola bilioni moja na milioni mia sita zimezingatiwa kwa ajili ya ustawi wa kiuchumi kwa miaka mitatu ya kwanza. Jamhuri ya Afrika ya Kati imekuwa ikikabiliwa na machafuko ya kidini na mapigano ya ndani katika kipindi cha miaka mitatu ya hivi karibuni suala ambalo limedhoofisha uchumi wa nchi hiyo.

Tags