May 02, 2024 02:37 UTC
  • Iran na Afrika ya Kati kuimarisha ushirikiano wa sekta ya madini

Waziri wa Biashara Ndogo na za Kati wa Afrika ya Kati ametangaza utayarifu wa nchi yake wa kushirikiana kikamilifu na Iran katika uchimbaji madini.

Angate Robard amesema pembezoni mwa Maonyesho ya Uwezo wa Kuuza Nje Bidhaa za Iran (Iran Expo 2024) mjini Tehran kwamba: Nchi yake iko tayari kujenga viwanda vya kuchakata madini, kuhamisha ujuzi na elimu ya ufundi na uhandisi kwa kushirikiana na Iran.

Angate Robard ameongeza kuwa: Jamhuri ya Afrika ya Kati ina migodi 400 inayojulikana kuanzia chokaa hadi metali mbalimbali zenye madini tofauti na inataka kushirikiana na Iran.

Waziri wa Biashara Ndogo na za Kati wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesisitiza kuwa: "Iran imefanyia kazi  rasilimali zake za madini, sisi pia tunatafuta washirika wa kibiashara na maarifa wa Iran."

Maonyesho ya 6 ya Iran ya mauzo ya bidhaa nje ya nchi, yanayojulikana kama Iran Expo 2024, yalianza hapa Tehran Aprili 27 na yanamalizika leo Mei 1.

Maonyesho hayo ni fursa nzuri ya kuarifisha bidhaa na huduma za Iran katika soko la kimataifa sambamba na kutambulisha utamaduni, sanaa na uwezo wa kisayansi wa nchi.

Tags