-
Waziri wa Afya wa serikali ya Taliban ya Afghanistan yupo ziarani nchini Iran
Sep 06, 2022 02:15Waziri wa Afya wa Serikali ya Taliban ya Afghanistan yupo ziarani hapa nchini Iran akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa serikali hiyo.
-
Mripuko wa kipindupindu waua makumi ya watu Kongo DR
Sep 01, 2022 07:34Mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu umepelekea watu wasiopungua 48 kupoteza maisha katika mkoa wa Sankuru, katikati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Iran inazalisha asilimia 98 ya dawa zake ndani ya nchi
Aug 27, 2022 11:17Shirika la Dawa na Chakula la Iran (FDA) limesema asilimia 98 ya dawa zilizoko nchini zinazalishwa na wataalamu wa taifa hili, na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ni miongoni mwa nchi 20 duniani zinazojizalishia dawa kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.
-
Nchi za Afrika zapasisha stratejia ya kupambana na magonjwa sugu
Aug 24, 2022 10:48Mawaziri wa Afya wa nchi za Afrika wameunga mkono stratejia mpya inayonuia kupiga jeki upatikanaji wa dawa na matibabu ya magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza barani humo.
-
Uhispania, Brazil zaripoti vifo vya kwanza vya Monkeypox nje ya Afrika
Jul 30, 2022 09:30Vifo vya kwanza vilivyotokana na ugonjwa wa Ndui ya Nyani (Monkeypox) nje ya bara la Afrika vimeripotiwa katika nchi za Uhispania na Brazil, huku maambukizi ya ugonjwa huo yakiongezeka kote duniani hususan barani Ulaya.
-
Afrika yalilia chanjo ya Monkeypox iliyoua watu 75 barani humo
Jul 30, 2022 03:43Afrika haina hata dozi moja ya chanjo ya kupambana na ugonjwa wa Ndui ya Nyani (Monkeypox), licha ya kuwa bara pekee lililosajili vifo vilivyotokana na maradhi hayo.
-
Marekani yaripoti kesi ya kwanza ya polio baada ya muongo mmoja
Jul 22, 2022 07:25Marekani imeripoti kesi ya kwanza ya ugonjwa wa kupooza au polio baada ya kupita karibu miaka kumi.
-
Afrika Kusini yasajili kesi ya kwanza ya ugonjwa wa Monkeypox
Jun 24, 2022 01:16Afrika Kusini imeripoti kesi ya kwanza iliyothibitishwa ya ugonjwa wa virusi wa Monkeypox.
-
Nchi 8 za Afrika miongoni mwa 39 duniani zilizoripoti Monkeypox
Jun 20, 2022 04:21Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema nchi 8 za Afrika ni miongoni mwa nchi 39 duniani zilizoripoti kesi zilizothibitishwa za ugonjwa wa Monkeypox.
-
Mripuko wa kipindupindu waikumba Cameroon, kesi 6,000 zaripotiwa
Apr 02, 2022 12:57Watu wasiopungua 100 wamepoteza maisha kutokana na mripuko mpya wa kipindupindu nchini Cameroon, huku wengine 6,000 wakikumbwa na ugonjwa huo.