-
WHO: Ebola imedhibitiwa katika vijiji vya Kongo DR
Oct 12, 2019 04:38Afisa wa ngazi za juu wa Shirika la Afya Duniani WHO amesema juhudi za kuvitokomeza kikamilifu virusi vya Ebola katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kong zinaendelea kuzaa matunda.
-
Umoja wa Afrika wataka ushirikiano katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola
Oct 04, 2019 08:32Umoja wa Afrika umetoa mwito wa kuwepo ushirikiano zaidi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya kuenea ugonjwa hatari wa Ebola.
-
Waliotibiwa ugonjwa wa Ebola wana hatari ya kukumbwa na maradhi ya figo na vifo vya haraka
Sep 05, 2019 21:58Watu waliookoka baada ya kutibiwa ugonjwa hatari wa Ebola wako katika hatari kubwa ya kufariki dunia kutokana na maradhi ya figo baada ya kupitisha mwaka mmoja tangu wanapotoka hospitalini. Taarifa hiyo ilitolewa jana Alkhamisi baada ya kufanyiwa uchunguzi watu hao nchini Guinea.
-
WHO yaipatia Uganda chanjo ya Ebola baada ya kifo cha mtoto
Aug 31, 2019 22:13Shirika la Afya Duniani (WHO) limeipati Uganda msaada wa dozi 300 za chanjo ya Ebola kwa ajili ya kuwapatia chanjo watu wote waliowasiliana na msichana mwenye umri wa miaka 9 aliyefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola katika wilaya ya Kasese inayopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Katibu Mkuu wa UN awasili Congo DR kujadili njia za kukabiliana na Ebola + Sauti
Aug 31, 2019 08:48Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewasili katika mji wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa Goma kwa shabaha ya kutathmini na kuchunguza njia za kukabiliana na ugonjwa hatari wa Ebola.
-
Kesi nyingine ya ugonjwa wa Ebola yathibitishwa nchini Uganda
Aug 30, 2019 22:32Wizara ya Afya ya Uganda imesema kuwa msichana mmoja mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amepatikana na virusi vya Ebola nchini Uganda. Wizara hiyo imesema kuwa, msichana huyo mwenye umri wa miaka 9, aliwasili nchini Uganda akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ingawa hata hivyo haikumtaja jina lake.
-
UNHCR: Hali ya elimu ya wakimbizi ni mbaya sana
Aug 30, 2019 22:17Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema kuwa, elimu ya wakimbizi iko hatarini na inaonesha kuwa kadiri watoto wakimbizi wanavyozidi kukua ndivyo vikwazo vya kupata elimu vinavyozidi kuongezeka.
-
Kesi ya pili ya Ebola nchini Uganda huku 2,000 wakipoteza maisha DRC
Aug 30, 2019 03:30Wizara ya afya ya Uganda imetangaza kesi ya pili ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola katika eneo la Kasese, kilomita 472 kutoka mji mkuu wa Kampala, baada ya mgonjwa mmoja wa Ebola kuingia nchini humo kutoka nchi jirani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Watu 200,000 wapata chanjo ya Ebola nchini DRC
Aug 25, 2019 21:48Watu zaidi ya 200,000 wamepata chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia (DRC) ya Kongo katika mwezi huu wa Agosti.
-
Burundi yaanza kutoa chanjo ya Ebola kwa wahudumu wa afya
Aug 15, 2019 07:32Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa serikali ya Burundi imeanza kutoa chanjo ya virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola kwa wahudumu wa afya hususan wale wanaofanyakazi karibu na mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.