Dec 13, 2019 08:04 UTC
  • Maambukizi ya ebola yaongezeka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema, maambukizi ya ugonjwa hatari wa ebola yameongezeka katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo.

Kufuatia kuongezeka maambukizi ya ebola, maafisa wa afya wa Kongo DR wamesema, katika kipindi cha siku tatu zilizopita, watu wengine 20 wamegundulika kupatwa na ugonjwa huo katika maeneo ya mashariki ya nchi.

Mripuko wa ugonjwa wa ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ulianza Mei 8 mwaka 2018 katika mji wa Bikoro mkoani Equater kaskazini magharibi mwa nchi na baadaye kuenea katika mji wa Mbandaka katikati mwa mkoa huo na pia mashariki mwa nchi hiyo.

Tangu mwaka 2014 hadi sasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeshakumbwa na miripuko mitatu ya ugonjwa wa ebola.

Kirusi cha ugonjwa huo hatari kimeshaua watu wapatao 11,000 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 katika maeneo mbali mbali duniani.../

Tags