-
Wanamgambo 50 wauawa na askari wa Ethiopia eneo la Amhara
Sep 26, 2023 13:02Wanamgambo wasiopungua 50 wameuawa katika makabiliano makali baina ya maafisa usalama wa serikali ya Ethiopia na genge moja la wanamgambo katika eneo la Amhara, kaskazini mwa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Ethiopia: Tumeanza duru mpya ya mazungumzo na Misri na Sudan kuhusu Bwawa Kuu la Renaissance
Sep 23, 2023 14:08Ethiopia imesema imeanza duru ya pili ya mazungumzo na Misri na Sudan kuhusu bwawa lenye utata lililojengwa na nchi hiyo kwenye mto Nile na kuwa chanzo cha mvutano wa muda mrefu kati ya mataifa hayo matatu.
-
Makumi ya wakimbizi wakufa njaa Gambella, Ethiopia
Sep 22, 2023 02:43Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Ethiopia (EHRC) imesema wakimbizi zaidi ya 30 wamepoteza maisha kutokana na njaa na utapiamlo katika jimbo la Gambella lililoko magharibi ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Jeshi la Ethiopia lasema limeua magaidi 462 wa al-Shabaab Somalia
Sep 22, 2023 02:41Kwa akali wanachama 462 wa kundi la kigaidi la al-Shabaab waliuawa mwisho mwa wiki nchini Somalia, Jeshi la Ulinzi la Taifa la Ethiopia (ENDF) limethibisha hayo na kueleza kuwa, magaidi hao waliuawa katika shambulizi lililotibuliwa katika kambi ya askari wa Ethiopia wanaohudumu chini ya Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS).
-
UN: Mauaji makubwa na uhalifu wa kivita unaendelea kufanywa Ethiopia
Sep 19, 2023 07:25Wataalamu huru wa haki za binadamu walioteuliwa na Umoja wa Mataifa wamesema, uhalifu wa kivita umeendelea kufanywa bila kusitishwa nchini Ethiopia karibu mwaka mmoja baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kufikiwa kati ya Serikali ya nchi hiyo na vikosi kutoka eneo la kaskazini la Tigray
-
Makumi ya wanajeshi wa Ethiopia wauawa katika hujuma ya kigaidi
Sep 18, 2023 07:44Makumi ya askari wa jeshi la Ethiopia wameuliwa katika shambulio la wanamgambo wa kundi la Shabab magharibi mwa Somalia.
-
Amnesty: Askari wa Eritrea walifanya jinai za kivita Tigray, Ethiopia
Sep 05, 2023 10:53Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema wanajeshi wa Eritrea waitifaki wa serikali ya Ethiopia walifanya jinai za kivita katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia.
-
UN: Watu 183 wameuawa katika mapigano Amhara, Ethiopia
Aug 30, 2023 08:16Umoja wa Mataifa umesema kwa akali watu 183 wameuawa katika mapigano yanayoendelea kushuhudiwa katika eneo la Amhara kaskazini mwa Ethiopia.
-
Baada ya vita na wanamgambo waasi, jeshi la Ethiopia linadhibiti tena miji mikubwa ya Amhara
Aug 10, 2023 07:25Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa imekomboa miji mikubwa katika eneo la Amhara kutoka kwa "magenge la wanamgambo waasi", baada ya siku kadhaa za vita kati ya jeshi la serikali kuu na wanamgambo wa eneo hilo.
-
Ethiopia yawatuhumu wanamgambo wa Amhara kuwa wanataka kupindua serikali
Aug 07, 2023 11:29Afisa wa ngazi ya juu wa Ethiopia amewatuhumu wanamgambo katika eneo la Amhara kuwa wanataka kupindua serikali za jimbo na ya shirikisho kufuatia mapigano ya siku kadhaa mtawalia ambayo yamepelekea mamlaka za uongozi kutangaza hali ya hatari.