Sep 18, 2023 07:44 UTC
  • Makumi ya wanajeshi wa Ethiopia wauawa katika hujuma ya kigaidi

Makumi ya askari wa jeshi la Ethiopia wameuliwa katika shambulio la wanamgambo wa kundi la Shabab magharibi mwa Somalia.

Shirika la habari la Mehr limeripoti kuwa, duru za habari za kundi la kigaidi la al Shabab zimetangaza kuwa kundi hilo limewauwa wanajeshi 167 wa Ethiopia huko magharibi mwa Somalia. 

Duru hizo za magaidi wa al Shabab zimeongeza kuwa, kundi hilo limewatia nguvuni wanajeshi wengine wa Ethiopia na kudai kuwa jeshi la Ethiopia limeshindwa kusonga mbele. Magaidi wa al Shabab wamedai kuangamiza zana na silaha za wanajeshi wa Ethiopia katika hujuma hiyo ya kigaidi.

Magaidi wa al Shabab 

Wanajeshi wa Ethiopia na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) hadi sasa hawajatoa taarifa yoyote kuhusu madai hayo ya kundi la al Shabab dhidi yao. 

Katika siku za karibuni jeshi la Ethiopia lilifanya jitihada kubwa kuimarisha kambi yao ya inayopatikana katika mji wa Wajd ambao unadhibitiwa na magaidi wa al Shabab kwa karibu muongo mmoja sasa. 

Tags