-
Ethiopia kuunganisha vikosi vya majimbo ya kikanda katika jeshi la taifa na polisi
Apr 10, 2023 08:05Serikali ya Ethiopia imesema kuwa inakusudia kujumuisha vikosi vyote maalumu vya majimbo ya kikanda ima katika jeshi la taifa, au polisi ya shirikisho au majimbo; hatua ambayo inaweza kuhesabiwa kama mpango wa kuyapunguzia mamlaka majimbo yanayosimamia mambo yake yenyewe.
-
Hafla kubwa zaidi ya futari yafanyika Ethiopia
Apr 09, 2023 08:00Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la Ethiopia limefanya hafla kubwa zaidi ya Iftar katika uwanja wa Al-Thaura mjini Addis Ababa, mji mkuu wa nchi hiyo, wakati huu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Ethiopia yaunda serikali ya mpito katika eneo la Tigray
Mar 24, 2023 03:40Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ametangaza habari ya kuundwa serikali ya mpito katika eneo la Tigray la kaskazini mwa nchi, kama sehemu ya utekelezaji wa makubakubaliano ya amani.
-
Bunge la Ethiopia limeiondoa harakati ya wapiganaji wa Tigray kwenye orodha ya magaidi
Mar 23, 2023 03:58Bunge la Ethiopia imeondoa katika orodha ya makundi ya kigaidi Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray TPLF ya kaskazini mwa nchi hiyo.
-
Tume ya Ethiopia: Waasi wa OLA wameua makumi ya raia 50 Oromiya
Feb 16, 2023 23:20Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Ethiopia (EHRC) imesema kwa akali raia 50 wameuawa na kundi la waasi linalojiita Jeshi la Ukombozi wa Oromo (OLA) katika eneo la Oromiya, magharibi mwa nchi.
-
Afwerki: Madai kwamba Eritrea imekiuka haki za binadamu Tigray, ni njozi tupu
Feb 09, 2023 23:24Rais wa Eritrea Isaias Afwerki jana Alhamisi aliyataja madai ya kukiukwa haki za binadamu kulikofanywa na wanajeshi wa Eritrea katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia wakati wa vita vya miaka miwili katika eneo hilo kuwa ni njozi tupu.
-
Shirika la ndege la Ethiopia kuanza tena safari zake huko Tigray
Dec 27, 2022 11:30Shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) limetangaza kuwa linaanza tena safari zake katika eneo la Tigray lililoathiriwa na machafuko huko kaskazini mwa Ethiopia sambambana eneo hilo kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme na kurejeshewa huduma za simu na nyinginezo.
-
Ethiopia yatuma ujumbe Tigray kwa ajili ya kutekeleza mapatano ya amani
Dec 26, 2022 23:01Ujumbe wa ngazi ya juu wa timu ya serikali ya Ethiopia umeelekea Tigray kaskazini mwa nchi hiyo kwa ajili ya mazungumzo ya kutekeleza makubaliano ya amani ili kuhitimisha mzozo wa miaka miwili kati ya serikali ya Addis Ababa na Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray (TPLF).
-
UN: Waliouawa Tigray, Ethiopia ni wengi zaidi ya waliouawa Ukraine
Dec 08, 2022 23:08Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema idadi ya watu waliouawa katika mapigano huko Tigray, kaskazini mwa Ethiopia ni wengi ikilinganishwa na idadi ya waliouawa katika vita vya Ukraine na Russia.
-
Tigray yaunganishwa tena kwenye gridi ya umeme ya taifa
Dec 07, 2022 22:51Makao makuu ya eneo la Tigray, Mekele, kwa mara nyingine tena yameunganishwa kwenye gridi ya umeme ya taifa baada ya kukosa umeme kwa zaidi ya mwaka moja kutokana na vita vilivyoliathiri eneo hilo la kaskazini mwa Ethiopia. Hayo yameelezwa na Kampuni ya Taifa ya Umeme ya nchi hiyo.