-
Waziri wa Gambia aihama serikali ya Rais Jammeh
Jan 10, 2017 16:26Waziri wa Mawasiliano wa Gambia Sheriff Bojang amesema ameamua kujiondoa kwenye serikali tangu rais Yahya Jammeh wa nchi hiyo alipokataa kuwa ameshindwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe mosi ya mwezi uliopita wa Desemba.
-
Mahakama kusikiliza ombi la Jammeh, Ecowas kurejea Gambia kesho
Jan 10, 2017 08:16Mahakama ya Kilele ya Gambia inatazamiwa hii leo kuanza kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais iliyowasilishwa na Rais Yahya Jammeh anayetaka matokeo ya uchaguzi yabatilishwe.
-
Nigeria: Viongozi wa ECOWAS kutoa 'uamuzi mkubwa' juu ya Gambia
Jan 07, 2017 08:06Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) wanatazamiwa hii leo kutoa kile kilichotajwa kuwa 'uamuzi mzito' kuhusiana na mgogoro wa kisiasa unaoikabili Gambia
-
Jeshi la Gambia latangaza kumuunga mkono Rais Yahya Jammeh
Jan 05, 2017 04:52Kamanda wa Jeshi la Gambia ametoa ujumbe akitangaza uungaji mkono kamili wa jeshi la nchi hiyo kwa Rais Yahya Jammeh ambaye amekataa kukabidhi madaraka ya nchi kwa njia ya amani baada ya kushindwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika nchini humo mwezi uliopita.
-
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Gambia akimbia nchi baada ya kutishiwa maisha
Jan 04, 2017 07:10Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Gambia amekimbia nchi akihofiwa usalama wake.
-
Mshindi wa uchaguzi nchini Gambia aitaka jumuiya ya ECOWAS imuondoe Jameh
Jan 03, 2017 13:48Mshindi wa uchaguzi wa rais uliomalizika hivi karibuni nchini Gambia, ameitaka Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS kutumia uwezo wake katika kumkinaisha Yahya Jammeh kukubali matokeo.
-
Gambia yafunga vituo viwili vya radio katika mgogoro wa baada ya uchaguzi
Jan 03, 2017 02:31Maafisa wa usalama Gambia wamefunga vituo viwili vya radio binafsi karibu na mji mkuu Banjul huku nchi hiyo ikikumbwa na mgogoro wa baada ya uchaguzi.
-
Kuendelea juhudi za kumshawishi Jammeh akabidhi madaraka kwa amani Gambia
Dec 29, 2016 02:44Mivutano ya kisiasa ya baada ya uchaguzi wa rais nchini Gambia ingali inaendelea huku Mahakama Kuu ya nchi hiyo ikisubiriwa kutangaza uamuzi wake kuhusiana na malalamiko yaliyowasilishwa na Rais Yahya Jammeh ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo.
-
Umoja wa Mataifa wamtaka Jammeh akabidhi madaraka Gambia
Dec 23, 2016 07:37Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemtaka Rais wa Gambia amkabidhi madaraka kwa amani Rais mteule wa nchi hiyo.
-
Mahakama Gambia kusikiza kesi ya uchaguzi Januari 10
Dec 22, 2016 06:56Mahakama ya Kilele ya Gambia imeakhirisha hadi Januari 10 mwakani kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais iliyowasilishwa na Rais Yahya Jammeh anayetaka matokeo ya uchaguzi yabatilishwe.