Mshindi wa uchaguzi nchini Gambia aitaka jumuiya ya ECOWAS imuondoe Jameh
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22750-mshindi_wa_uchaguzi_nchini_gambia_aitaka_jumuiya_ya_ecowas_imuondoe_jameh
Mshindi wa uchaguzi wa rais uliomalizika hivi karibuni nchini Gambia, ameitaka Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS kutumia uwezo wake katika kumkinaisha Yahya Jammeh kukubali matokeo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 03, 2017 10:18 UTC
  • Mshindi wa uchaguzi nchini Gambia aitaka jumuiya ya ECOWAS  imuondoe Jameh

Mshindi wa uchaguzi wa rais uliomalizika hivi karibuni nchini Gambia, ameitaka Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS kutumia uwezo wake katika kumkinaisha Yahya Jammeh kukubali matokeo.

Adama Barrow, amesema kuwa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS kwa pamoja zinatakiwa kutumia nafasi zao katika kuhakikisha katiba ya Gambia inaheshimiwa.

Rais Jammeh akiwa na wapambe wake

Kabla ya hapo ECOWAS ilitangaza kumteua Rais Muhammadu Buhari wa Nigenia kuwa mpatanishi wa pande za kisiasa nchini Gambia. Rais Yahya Jammeh ambaye amekuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 22 alishindwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwanzoni mwa mwezi Disemba mwaka jana na kukubali matokeo yaliyompa ushindi hasimu wake Adama Barrow.

Adama Barrow, mshindi wa uchaguzi Gambia

Hata hivyo siku chache baadaye aliibuka na kutilia shaka matokeo hayo sanjari na kukataa kuondoka madarakani.