-
Droni ya Imarati yatunguliwa nchini Libya
Jun 02, 2019 23:48Jeshi la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya limetangaza kuwa, limefanikiwa kutungua ndege moja isiyo na rubani (droni) ya serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.
-
Baraza la Kiislamu Uswisi: Imarati inayaunga mkono makundi yaliyo dhidi ya Uislamu barani Ulaya
May 27, 2019 22:40Mkuu wa Baraza la Kiislamu nchini Uswisi ameelezea nafasi haribifu ya Umoja wa Falme za Kiarabu (IMARATI) katika kuviunga mkono vyama na makundi yanayoendesha harakati na kampeni dhidi ya dini ya Uislamu.
-
Yemen: Tunao uwezo wa kukwamisha kazi za viwanja vya ndege vya Abu Dhabi na Riyadh
May 25, 2019 21:59Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la harakati ya Answarullah ya Yemen amesema kuwa, kurushwa hewani video inayoonesha kushambuliwa uwanja wa ndege wa Abu Dhabi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ni ushahidi wa nguvu za kijeshi za kujihami wananchi wa Yemen kama ambavyo pia ni ushahidi kwamba Wayemen wanao uwezo wa kukwamisha kazi za viwanja vya ndege vya Riyadh na Abu Dhabi.
-
Trump aziuzia Saudia, UAE silaha za dola bilioni 8 bila idhini ya Kongresi ya Marekani
May 25, 2019 03:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amethibitisha kuwa serikali ya Washington imeidhinisha mauzo ya silaha zenye thamani ya dola bilioni 8.1 kwa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, bila idhini ya Kongresi ya nchi hiyo.
-
Saudia na Imarati kushiriki mkutano wa Marekani dhidi ya Palestina
May 22, 2019 21:58Tawala vibaraka za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu zimetangaza kuwa zitashiriki mkutano wa Marekani wa kuzindua hatua ya mwanzo ya utekelezaji wa 'Muamala wa Karne' mwezi ujao wa Juni nchini Bahrain.
-
Jamhuri ya Kiislamu yataka kuwekwa wazi kiundani tukio la bandari ya Fujairah nchini Imarati
May 13, 2019 09:49Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Tehran imesikitishwa na matukio ya jana Jumapili yaliyotokea dhidi ya meli kadhaa za mafuta katika Bahari ya Oman katika eneo la Umoja wa Falme za Kiarabu na imetaka kuwekwa wazi na kwa kina uhakika wa matukio hayo.
-
Somalia yasambaratisha mtandao wa majasusi wa UAE
May 11, 2019 08:25Wakuu wa Somalia wametangaza kuusambaratisha mtandao wa majasusi ambao walikuwa wakiutumikia utawala wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
-
Kuongezeka mvutano kati ya Imarati na serikali iliyojiuzulu ya Yemen
May 10, 2019 03:12Umoja wa Falme za Kiarabu, Imarati, ambayo iko katika muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita vyake vya kivamizi dhidi ya Yemen, imeingia katika mvutano mkubwa kati yake na serikali iliyojiuzulu ya Yemen ambayo hivi sasa ingali inadhibiti eneo la kusini mwa nchi hiyo.
-
UN: Yumkini Imarati imehusika katika mashambulizi ya Libya
May 07, 2019 03:26Jopo la Wataalamu wa Umoja wa Mataifa linatathmini mashambulizi ya makombora dhidi ya mji mkuu wa Libya, Tripoli, sanjari na kuchunguza uwezekano wa kutumika ndege zisizo na rubani 'drone' za Umoja wa Falme za Kiarabu katika hujuma hizo.
-
Mwanamke mwenye saratani afia gerezani Imarati licha ya indhari ya UN
May 05, 2019 09:49Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeripoti kuwa, mwanamke aliyekuwa anaugua ugonjwa wa saratani amepoteza maisha akiwa gerezani katika Umoja wa Falme za Kiarabu, miezi miwili baada ya Umoja wa Mataifa kutoa mwito wa kuachiwa huru mwanamke huyo kwa misingi ya kwenda kupatiwa matibabu.