-
Waislamu Indonesia walaani uepo wa Israel Kombe la Dunia U20
Mar 21, 2023 02:28Wananchi Waislamu wa Indonesia wamefanya maandamano ya kulalamikia hatua ya kuruhusiwa utawala haramu wa Israel kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia katika mchezo wa kandanda kwa vijana wa kiume wenye umri usiozidi miaka 20.
-
Hatimaye Waislamu Warohingya wawasili pwani ya Indonesia baada ya kutaabika baharini kwa mwezi mzima
Dec 26, 2022 02:17Makumi ya Waislamu wakimbizi wa jamii ya Rohingya kutoka Myanmar waliodhoofu kwa njaa na kiu wamepatikana ufukweni mwa pwani ya jimbo la Aceh kaskazini ya Indonesia baada ya wiki kadhaa za kutaabika na kutangatanga baharini.
-
Indonesia yakataa kumpokea mjumbe maalumu wa kutetea ubaradhuli wa Marekani
Dec 03, 2022 10:44Marekani imelazimika kufuta safari ya mjumbe wake maalumu wa kutetea eti haki za mabaradhuli (LGBTQ) nchini Indonesia, baada ya nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia kusema kuwa haitampokea afisa huyo wa Washington.
-
Mtetemeko wa ardhi waua watu 162 nchini Indonesia
Nov 22, 2022 02:37Watu zaidi ya 160 wanaripotiwa kupoteza maisha nchini Indonesia baada ya kutokea mtetemeko wa ardhi katika eneo la Cianjur, mkoa wa Java Magharibi.
-
174 waaga dunia katika mkanyangano kwenye uwanja wa soka Indonesia
Oct 02, 2022 07:34Kwa akali watu 174 wamepoteza maisha baada ya mashabiki wa timu hasimu za mpira wa miguu kushambuliana katika uwanja wa soka nchini Indonesia.
-
Marais wa Iran na Indonesia wasisitiza kupanua uhusiano katika nyanja mbalimbali
May 05, 2022 02:44Marais wa Iran na Indonesia wamefanya mazungumzo ya simu wakijadili uwezo wa nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali na kusisitiza ulazima wa kufanyika juhudi za pamoja za kuboresha kiwango cha ushirikiano wa pande mbili.
-
Waindonesia waandamana kulaani uungaji mkono wa US kwa Israel
May 28, 2021 12:31Wananchi wa Indonesia wamefanya maandamano nje ya ubalozi wa Marekani na ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Jakarta kulalamikia na kulaani uungaji mkono wa Marekani kwa jinai za utawala haramu wa Israel.
-
Hakuna matumaini ya kuwapata hai watu 53 katika nyambizi iliyozama ya Indonesia
Apr 25, 2021 06:37Maafisa wa Indonesia wamesema mabaki ya nyambizi ya nchi hiyo iliyotoweka siku chache zilizopita yamepatikana, na hivyo matumaini ya kuwakuta wakiwa hai mabaharia 53 kwenye chombo hicho yamefifia kikamilifu.
-
Makumi wafariki dunia kutokana na mafuriko, maporomoko ya ardhi Indonesia
Apr 04, 2021 12:50Makumi ya watu wamepoteza maisha na wengine wengi hawajulikani walipo baada ya kutokea mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Indonesia.
-
Indonesia yathibitisha kuanguka baharini ndege iliyokuwa imebeba abiria 62
Jan 10, 2021 08:18Wizara ya Uchukuzi ya Indonesia imethibitisha kuwa, ndege ya abiria ya nchi hiyo ambayo iliripotiwa kupoteza mawasiliano muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Jakarta, imeanguka baharini ikiwa na abiria 62 wakiwemo watoto 10.