-
Abdollahian: Iraq ina wajibu wa kuzuia vitisho dhidi ya Iran kutokea Kurdistan
Nov 15, 2022 04:08Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa mwito kwa jirani yake Iraq kuchukua hatua za kuzuia vitisho vinavyopangwa na kutekelezwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kutokea eneo lenye mamlaka ya ndani la Kurdistan, kaskazini mwa Iraq.
-
Tehran yalaani vikwazo vipya vya EU dhidi ya Iran
Nov 15, 2022 03:52Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikwazo vipya vilivyotangazwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya shakhsia 29 na taasisi tatu za Kiirani, ikiwemo kanali ya televisheni ya Press TV.
-
Timu ya kandanda ya Iran yawasili Qatar kushiriki Kombe la Dunia
Nov 15, 2022 00:19Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewasili Doha, mji mkuu wa Qatar kwenda kuweka kambi ya kujianjdaa kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza kutifua mavumbi wiki ijayo.
-
Mousavi: Droni za maadui zipo ndani ya shabaha ya mfumo wa Bavar 373
Nov 14, 2022 03:16Kamanda wa Majeshi ya Iran amesema ndege zisizo na rubani za maadui zipo ndani ya shabaha ya mfumo wa makombora ya kujihami ya masafa marefu wa Bavar 373.
-
Bidhaa za Iran zinazidi kupata umaarufu barani Afrika
Nov 13, 2022 01:11Kaimu Mkuu wa Kituo cha Biashara ya Iran na Afrika amesema: "Inatabiriwa kuwa kwa kasi ya sasa ya ustawi wa biashara ya Iran na Afrika katika mwaka huu (1401 Hijria Shamsia) kiwango cha mauzo ya bidhaa za Iran barani Afrika kitafika dola bilioni 1.8.
-
Mashinikizo mapya ya Magharibi dhidi ya Iran baada ya kushindwa mradi wa kuibua ghasia
Nov 12, 2022 22:52Nchi za Magharibi baada ya kushindwa mradi wao wa kuibua ghasia nchini Iran sasa zinatafuta njia nyingine mpya mbadala ili kuiwekea mashinikizo Tehran. Katika uwanja huo, nchi za Magharibi khususan za Ulaya mbali na kuratibu vikwazo vipya zimejielekeza katika kutoa taarifa na maazimio dhidi ya Iran sambamba na kushadidisha mashinikizo ya kisiasa dhidi ya nchi hii.
-
Jitihada za kufunga kituo cha Kiislamu cha Hamburg, Ujerumani
Nov 12, 2022 08:48Katika juhudi za madola ya Magharibi za kuunga mkono ghasia na machafuko nchini Iran, vyama vya muungano unaotawala nchini Ujerumani vimetoa wito wa kufungwa Kituo cha Kiislamu na Kiutamduni cha Iran katika mji wa Hamburg nchini humo.
-
Amir Abdollahian: Azimio la UN haliizuia Iran kuuza silaha nje ya nchi
Nov 12, 2022 04:40Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema: "Kwa mujibu wa azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama, hakuna marufuku ya kuagiza na kuuza silaha za Iran nje ya nchi, na Tehran haijaipa Russia silaha zozote ili zitumike katika vita vya Ukraine."
-
Faili la pili la sauti ya mwandishi wa BBC: Lengo la ghasia ni kuigawa Iran
Nov 11, 2022 04:37Faili la pili la sauti lililovuja la mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limefichua wazi zaidi jinsi televisheni inayofadhiliwa na Saudia inayojiita 'Iran International' inavyoongoza kampeni ya kuigawa Iran vipande vipande.
-
Iran yaionya Ujerumani: Jibu letu kwa uingiliaji wenu litakuwa zito
Nov 10, 2022 07:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali matamshi ya uingiliaji na ya kichochezi yaliyotolewa na mwenzake wa Ujerumani na kuonya kuwa, Tehran itatoa jibu lenye mlingano na madhubuti kwa misimamo hiyo ya uingiliaji wa masuala ya ndani ya nchi hii.